Kumbukumbu za mwezi wa Ramadhani: Mwezi kumi Ramadhani alifariki mama wa Waumini bibi mtakasifu Khadija bint Khuwailid (r.a)...

Maoni katika picha
Mwezi mtukufu wa Ramadhani unamatukio mengi ya kihistoria, miongoni mwake kuna ya kufurahisha na ya kuhuzunisha na kuumiza, miongoni mwa matukio ya kuumiza kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) ni kufariki kwa mama wa Waumini na mke mtukufu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) bibi Khadijatu Kubra (r.a), ambaye alifariki mwezi kumi Ramadhani, mwaka wa kumi wa Utume na miaka mitatu kabla ya Mtume kuhama Maka na kwenda Madina (Hijra), bibi huyu mtukufu aliondaka hapa duniani na kumuachia Mtume (s.a.w.w) maumivu makubwa sana katika moyo wake na umma wa kiislamu kwa ujumla, alikua ngome muhimu kwake, kilicho zidisha huzuni kwa Mtume (s.a.w.w) alikufa mwaka alio fariki Ammi yake Abu Twalib (r.a) aliye kua ngome yake kisiasa na kijamii, hivyo Mtume hakuusahau mwaka huo katika maisha yake yote na aliuita “mwaka wa huzuni”.

Mama wa Waumini bibi Khadija bint Khuwailid (r.a) jina lake ni: Khadija bint Khuwailid bun Asad bun Abdul-Uza bun Quswai Alquraishiy Al-Asadiy alipewa jina la sifa (laqabu) la Twahirah, alikua mwanamke bora wa kikuraishi na Maka kwa ujumla kwa sura na tabia, alikua na vipaji vingi, akili, hekima na utajiri, Shekh Majlisiy muandishi wa kitabu cha Bihaar ameandika kua; alikua na nyumba inawatosha watu wote wa Maka kipindi kile, Bibi Khadija alikua mtu wa kwanza kumuamini Mwenyezi Mungu mtukufu, imepokewa kutoka kwa Ibun Abbasi anasema kua: “Mtu wa kwanza kumuamini Mtume (s.a.w.w) katika wanaume ni Ali (a.s) na katika wanawake ni Khadija (r.a)”, alivumilia pamoja na Mtume (s.a.w.w) mateso waliyo yapata kutokana na ujumbe wa Mwenyezi Mungu mtukufu, alishirikiana naye katika raha na shida, alivumilia tabu kubwa ya maisha baada ya waarabu kuwakatia huduma, akajitolea mali zake zote, hakika ni mfano wa pekee wa mwanamke mu-umin, hakika bibi Khadija baada ya kuolewa na Mtume (s.a.w.w) alikua ngome muhimu sana kwa Mtume katika kupambana na mitihani ya Utume, alimpunguzia matatizo aliyo kua akifanyiwa na makafiri wa kikuraishi.

Aliolewa (r.a) na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) mwezi kumi Rabiul Awwal, akiwa na miaka arubaini, na Mtume (s.a.w.w) akiwa na miaka ishirini na tano, Mtume hakuoa mke mwingine hadi bi Khadija alipo fariki, wanachuoni wametofautiana kuhusu idadi ya watoto alio zaa na Mtume (s.a.w.w) lakini wote wamekubaliana kua Kassim na bibi Fatuma Zaharaa (a.s) ni miongoni mwa watoto wake, Kassim alifariki wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w) na Mtume alikua akiitwa baba Kassim.

Bibi Khadija (r.a) ana nafasi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) anasema: (Wanawake bora duniani ni wanne: Maryam bint Imraan, Assia mwanamke wa Fir’aun, Khadija bint Khuwailid na Fatuma bint Muhammad).

Bibi Khadija alipo fariki, Mtume (s.a.w.w) alimuosha na kumpamba, alipo taka kumvisha sanda Jibrilu (a.s) akaja na akasema: (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.. Hakika Mwenyezi Mungu amekutumia salamu na anakuambia: Ewe Muhammad hakika sanda ya bi Khadija inatoka kwetu, hakika alitumia mali zake katika njia yetu). Jibrilu akaja na sanda na akasema: (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sanda ya bi Khadija hii hapa, nayo imetoka peponi Mwenyezi Mungu amemzawadia).

Mtume (s.a.w.w) akamvisha shuka yake tukufu kwanza, kisha akamvisha sanda aliyo letewa na Jibrilu (a.s), akawa kavishwa sanda mbili: sanda kutoka kwa Mwenyezi Mungu na sanda kutoka kwa Mtume, alikufa akiwa na umri wa miaka (65) na akazikwa katika makaburi ya Hajuun katika mji mtukufu wa Maka, Mtume (s.a.w.w) akaingia kumlaza ndani ya kaburi lake, wakati huo swala ya jeneza haikuwepo katika uislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: