Atabatu Abbasiyya tukufu yafungua kituo cha utamaduni cha kutoa mafunzo ya kimaendeleo katika wilaya ya Sanjaar…

Maoni katika picha
Kufuatia kuingia mwezi wa Rahma na Maghfirah, mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kutokana na ujumbe wake wa kidini na kimaadili, kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza uzinduzi wa kituo cha utamaduni katika wilaya ya Sanjaar iliyopo mkoani Mosul, nacho kitakua kituo cha kwanza cha dini kufunguliwa tangu kukombolewa kwa mji huo kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, na huu utakua mwanzo wa kuelekea kufungua miradi mingine na sehemu ya kuwakusanya watu wa tabaka zote wakazi wa mji wa Sanjaar.

Rais wa kitengo tajwa hapo juu Shekh Swalahu Karbalai ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tangu kukombolewa kwa wilaya ya Sanjaar Atabatu Abbasiyya tukufu imekua mstari wa mbele kutoa misaada bila ubaguzi kwa watu wa mji huu, tumefanya misafara mingi ya kuja kutoa misaada, wakati wa vita ya kukomboa mji huu, kamati ya misaada ya Atabatu Abbasiyya ilisimama imara kutoa misaada kwa wapiganaji watukufu, hivyo mji huu sio mgeni kwetu, kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mji huu kifikra na kitamaduni katika hali inayo endana na misingi ya dini ya kiislamu, ambayo ni dini ya maelewano na ubinadamu tumeamua kufungua kituo hiki”.

Akaongeza kusema kua: “Kituo hiki kinamajukumu mengi, ikiwa ni pamoja na kufanya mihadhara na vikao vya usomaji wa Qur’an pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiliamali, na mambo mengine ambayo faida yake inarudi kwa wakazi wa Sanjaar, hakika kituo kimesha anza kutekeleza majukumu yake kupitia Shekh Haidari Aaridhiy, ambaye anatoa mihadhara ya kidini na anaongoza swala ya jamaa pamoja na harakati zingine zinazo endana na mwezi mtukufu wa Ramadhani, kapata mwitikio mkubwa kutoka kwa wakazi wa mji huu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: