Kwa kusoma vikundi vinne, vimekamilisha mzunguko wa pili ya mashindano ya Qur’an ya vikundi awamu ya nne, yanayo simamiwa na kituo cha kuandaa wasomaji na mahafidhi katika Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, katika mwezi wa Ramadhani ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Hatua hii ilishuhudia mchuano mkali baina ya vikundi nane, vilivyo kua vikuchuana kwa karibu toka hatua ya kwanza, yalikua na uzuri wa aina yake kuanzia uulizaji wa maswali na ujibuji wake, pamoja na mwitikio mkubwa wa mazuwaru walio onyesha furaha zao wakati wakifuatilia mashindano haya.
Walio ingia katika mzunguko wa tatu ni; kikundi cha Waaswit, Diwaniyya, Najafu na Hashdi Sha’abi.
Kumbuka kua mashindano yana hatua (4), na vikundi vinavyo shiriki ni zaidi ya (16) kutoka katika mikoa mbalimbali, kila kikundi kina (Msomaji, Mfasiri na Haafidh), mashindano yameendeshwa na kamati iliyo bobea katika sekta hii, kamati hiyo inajukumu la kuandika max na kutangaza washindi, mashindano haya yanaendelea hadi mwezi (15) Ramadhani, na yanafanyika kila siku.