Kumbukumbu za mwezi wa Ramadhani: Mwezi kumi na mbili Ramadhani ni siku ambayo Mtume aliunga undugu baina ya Muhajirina na Answari na baina yake na ndugu yake mtoto wa Ammi yake Ali…

Maoni katika picha
Hongera kwa Muhajirina, kwa uhusiano uliojengwa kwa misingi ya imani, haki na undugu ulio onekana katika mahusiano yao, ukawa ni msingi wa kujenga jamii ya kiislamu yenye mshikamano kwa ajili ya kutangaza ujumbe wa Mwenyezi Mungu mtukufu.

Kazi ya kwanza aliyo fanya Mtume (s.a.w.w) baada ya kujenga msikiti ilikua ni kuunga undugu baina ya Muhajirina na Answari, ulio jengwa juu ya msingi wa imani na upendo wa dhati, kwa ajili ya kusaidiana na kulindana, na kupeana mali na starehe, kiunganishi kikubwa kilikua ni kuunga undugu, Mtume (s.a.w.w) aliunga undugu baina ya Muhajirina kabla ya kuhama, wakiwa bado wako Maka, na baada ya kuhamia Madina akaunga undugu baina ya Muhajirina na Answari.

Mtume (s.a.w.w) alipo unga undugu baina ya maswahaba wake, Kiongozi wa Waumini Ali bun Abu Twalib alikwenda kwa Mtume yakiwa macho yake yanalengalenga machozi, akasema (a.s): (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu umeunga undugu baina ya maswahaba wote, na wala hauja unga undugu baina yangu na yeyote?) Mtume (s.a.w.w) akasema: (Ewe Ali.. Hauridhiki mimi kua ndugu yako?) akasema (a.s): (Hapana ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ninaridhika). Kisha Mtume (s.a.w.w) akasema: (Wewe ni ndugu yangu Duniani na Akhera).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: