Kwa ajili ya kunufaika na kipindi cha likizo: Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel yaanza kusajili washiriki wa program ya pili ya Skaut (PDC)…

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kunufaika na kipindi cha likizo za kiangazi, Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel ambayo uko chini ya idara ya watoto katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza usajili wa awamu ya pili ya program ya mafunzo ya Skaut (PDC), kuanzia watoto wa miaka tisa hadi kumi na nane, kila hatua itakua na program yake zinazo endana na umri wa washiriki.

Program hii itadumu kwa muda wa miezi miwili na nusu, itakua na ratiba mbalimbali za mafunzo, miongoni mwa ratiba hizo ni:

  • 1- Mafunzo ya dini, kuhusu Akhlaq, Ubinadamu na hukumu za kifiqhi.
  • 2- Mafunzo ya kumuandaa kiongozi na kuibua vipaji na uwezo wa akili.
  • 3- Mafunzo ya namna ya kuandaa hema za Skaut na kila kinacho husu kujitegemea na kufanya kazi kama timu moja.
  • 4- Mafunzo ya uana habari kwa ujumla.
  • 5- Mafunzo ya ujasiliamali na kuinua kiwango cha uwelewa wa mambo ya utamaduni.
  • 6- Kufanya mashindano mbalimbali ya michezo, kama vile mpira wa miguu na mingineyo.
  • 7- Kujenga moyo wa umoja na kufanya kazi kama tim moja.
  • 8- Kuongeza kiwango cha elimu kwa wanachama na kuibua vipaji vyao.

Kwa wanaopenda kushiriki na wanao ishi katika mji wa Karbala na vitongoji vyake wafike katika jengo la Imamu Hassan (a.s) lililokua likijulikana kama -hoteli ya Dallah- lililopo katika mlango wa Bagdadi (Babu Bagdadi), kwa maelezo zaidi piga simu namba (07602326690), kumbuka kua nafasi ni chache na mwisho wa usajili ni 20/06/2018m.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: