Mashindano ya Qur’an ya vikundi yanayo fanyika chini ya usimamizi wa kituo cha miradi ya Qur’an katika Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya yamefika hatua ya mwisho, baada ya kumaliza hatua ya tatu, na walioingia katika fainali ni kikundi cha mkoa wa Najafu na Waasit, na kikundi cha Diwaniyya na Hashdi Sha’abi watachuana katika kushindania nafasi ya tatu na ya nne.
Mashindano haya yalianza tangu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, na yalikua na ushindani mkubwa sana, mara nyingi matokeo yaligongana au yalikaribiana, jambo hili linaonyesha ubora wa vituo vya Qur’an.
Kumbuka kua mashindano haya yana mizunguko (4) na vikundi washiriki vipo zaidi ya (16) kutoka katika mikoa tofauti, kila kikundi kina (msomaji, mfasiri na haafidh), mashindano yaha yanaendeshwa chini ya kamati ya majaji walio bobea katika fani za Qur’an, hao ndio wanao husika na kuuliza maswali kwa kufuata utaratibu ulio pangwa na ndio watakao tangaza matokeo, mashindano yanafanyika siku (15) mfululizo jioni.