Kufuatia muendelezo wa kazi za kiutalamu: Kituo cha uzalishaji na matangazo ya moja kwa moja Alkafeel chazindua filamu ya bibi Khadija (r.a)…

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kifo cha mama wa waumini na mke mtukufu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) bibi Khadijatu Kubra (r.a), kituo cha uzalishaji na matangazo ya moja kwa moja Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kimezindua filamu iitwayo (Bibi wa Makuraish), filamu yenye picha zenye muonekano mzuri, makini na yenye maelezo sahihi yaliyo toka katika vitabu vikubwa na tegemezi vya waislamu, falamu hii imetengenezwa kwa ajili ya kuelezea maisha ya bibi huyu mtukufu ambaye historia haija mtendea haki.

Filamu hii ni sehemu ya filamu za vielelezo zinazo tolewa na kituo hiki, kama vile filamu ya (Mkuu wa maswahaba) na (Maaliki Ashtari) na zinginezo, inaangazia baadhi ya matukio muhimu aliyo fanya mama huyu mpiganaji katika uhai wake, na inamuda wa dakika (27) ishirini na saba, picha za filamu hii zimepigwa Iran, Lebanon, Sirya pamoja na maeneo mengine ambayo msanifu wa filamu aliona yanafaa, waigizaji wa filamu hii ni watu walio bobea katika fani hiyo kutoka ndani na nje ya Iraq.

Taarifa za kihistoria zilizomo ndani ya filamu hii zimetolewa katika vitabu tegemezi vya hadithi na historia (vya kisunni na kishia), kisha taarifa hizo ziliwasilishwa katika kamati ya wasomi wakazifanyia uhakiki wa kihistoria na usalama wake kifikra, filamu imepambwa na baadhi ya mahojiano na viongozi wa dini kutoka ndani na nje ya Iraq, kila mmoja amemzungumzia bibi huyu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: