Atabatu Abbasiyya tukufu yaingiza katika mfumo wake wa viyoyozi tani (860) za viyoyozi…

Maoni katika picha
Mafundi wanao fanya kazi katika idara ya viyoyozi chini ya kitengo cha uangalizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutegemea utalamu wao binafsi, bila msaada ya watalamu wa nje, wameongeza tani (860) za viyoyozi katika mfumo mkuu wa viyoyozi vya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ongezeko hili limefanywa kutokana na kuongezeka joto, na kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kufanya ibada kwa mazuwaru, pia kufuatia upanuzi wa majengo unao shuhudiwa katika Ataba tukufu, kama vile ujenzi wa kumbi za chini ya harama (sardabu) tukufu, na upanuzi wa maeneo mapya, kwa upange mwingine ongezeko hili linasaidia kuwepo kwa viyoyozi vya hakiba, vinavyo weza kusaidia wakati wowote litakapo tokea tatizo la kuharibika au kusimama kufanya kazi kwa mfumo mkuu wa viyoyozi.

Kazi ya ufungaji wa mitambo ya viyoyozi ilitanguliwa na kazi za awali, kama vile kubaini maeneo ya kufungwa viyoyozi hivyo na kuandaa michoro kamili, kisha ndio kazi ya kufunga viyoyoti ikaanza, hadi sasa zimesha fungwa tani (430) za viyoyozi vya aina ya (CLIMAVENETA) pamoja na viambatanishi vyake vyote ukiwemo umeme, tayali yamesha fanyika matengenezo muhimu ya usambazaji wa mabomba kutokana na mahitaji ya mitambo mipya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: