Miongoni mwa ratiba za kongamano la Kariimu Ahlulbait (a.s) la kumi na moja: Ni kutoa zawadi kwa baadhi ya familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi…

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s) na katika ratiba ya kongamano la mwaka wa kumi na moja la Kariimu Ahlulbait (a.s), Uongozi mkuu wa Atabatu Kadhimiyya kwa kushirikiana na kamati kuu ya miradi ya Hilla mji wa Imamu Hassan (a.s) na taasisi ya kijamii ya Ain, wamefanya mahafali maalumu ya kuwapa zawadi baadhi ya wanafamilia wa mashahidi wa Hashdi Sha’abi, katika sehemu ya -Maqamu Radu Shamsi- na kuhudhuriwa na watu wengi kutoka sehemu tofauti.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano, Ustadh Muhandisi Hassan Alhilliy ametuelezea kuhusu mahafali hii kua: “Hafla ya kutoa zawadi inasimamiwa na Atabatu Kadhimiyya tukufu kwa mwaka wa nne mfululizo, ni miongoni mwa ratiba muhimu iliyo pangwa na kamati ya maandalizi ya kongamano tangu kuanza kwa vita ya kuikomboa Iraq, kutokana na maagizo ya Marjaa dini mkuu yanayo sisitiza kuzijali familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi, walio jitolea kwa hali na mali na wakajitolea hadi roho zao kwa ajili ya taifa hili tukufu, na walikua ngome imara dhidi ya magaidi, uongozi mkuu wa Atabatu Kadhimiyya kwa kushirikiana na tawi la taasisi ya kijamii ya Ain lililopo katika mkoa wa Baabil wamefanya hafla ya kuwapa zawadi baadhi ya familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi”.

Akaongeza kusema kua: “Hafla hiyo ilikua na vipengele vingi, baada ya kusoma Qur’an tukufu na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu, kulikua na neno ya ukaribisho, lililo tolewa na Ustadh Abduridha Mukhiif naibu rais wa kamati kuu ya miradi ya Hilla mji wa Imamu Hassan (a.s), kisha ukafuata upandishaji wa bendera za Maimamu wawili Jawadaini (a.s) katika sehemu ya Maqamu tukufu. Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa Atabatu Kadhimiyya ulio wasilishwa na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi Ustadh Muhammad Bannaau, akaelezea hadhi ya mashahidi na kwamba wao ni kielelezo cha ukamilifu na utukufu, ni wasila kubwa na lengo muhimu, ni njia fupi ya kumfikisha mwanadamu katika kilele cha utukufu, ni mlengo wa uhai mtukufu, ni ahadi ya mawalii na utekelezaji wa mawasii.. nayo ni moja ya mambo makubwa katika maisha ya mwanadamu, ni jambo kubwa linalo mpa ukamilifu, kwani linatendeka kwa mapenzi, kujitolea na uaminifu, na limepambwa na maadili mema zaidi ya kiubinadamu, akaongeza kusema kua: yatupasa tumshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu na tuwashukuru na kuwapongeza wapiganaji wetu wa Hashdi Sha’abi kwa ushindi walio pata katika uwanja wa vita, hakika walipigana vita tukufu na kali mno, wala hawakupigana kwa ajili ya kulinda maeneo matukufu peke yake, bali walipigana kwa ajili ya uzalendo wao katika taifa hili”.

Akaendelea kusema kua: “Hali kadhalika Shekh Imaad Kadhimiy rais wa kitengo cha dini alitoa muhadhara wa dini, akabainisha hadhi na nafasi ya familia za mashahidi, na jukumu alilo nalo kila mtu kuhusu familia hizo, hakika walijitolea kila walicho nacho hadi roho zao kwa ajili ya kulinda taifa hili na maeneo matukufu, pia hafla ilipambwa na kaswida kutoka katika kikosi cha waimbaji cha Atabatu Kadhimiyya, na mwisho wa hafla familia za wanajihadi zikapewa zawadi ya hela na vitu vingine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: