Kufungwa pazia la mashindano ya Qur’an ya vikundi ya nne kwa ushindi wa kikundi cha Waasit…

Maoni katika picha
Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umeshuhudia kuhitimishwa kwa mashindano ya Qur’an ya vikundi yanayo simamiwa na kituo cha miradi ya Qur’an kilichopo ndani ya Maahadi ya Qur’an chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuhudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar na jopo la viongozi wengine, kikundi cha mkoa wa Waasit kimepata nafasi ya kwanza huku kikundi cha mkoa wa Najafu kikipata nafasi ya pili, na kikundi cha Hashdi Sha’abi kimepata nafasi ya tatu huku kikundi cha mkoa wa Diwania kikiambulia nafasi ya nne.

Mashindano haya yalianza tangu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na yalikua na mchuano mkali sana kiasi matokeo yalikua yanakaribiana sana katika mizunguko yote ya mashindano haya, hakika kulikua na ushindani wa wazi na kila kikundi kilijipanga kuchukua ushindi.

Baada ya kuhitimisha mashindano haya kikundi kilicho shinda kikapewa zawadi, washindi wa kwanza amepewa bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) ambayo watakaa nayo kwa muda wa mwaka mmoja, na safari ya kwenda Umra katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, washindi wa pili wamepewa midani ya dhahabu, huku washindi wa tatu wakipewa bendera iliyo fanyiwa tabaruku katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kua mashindano haya yalikua na mizunguko (4), na vikundi washiriki vilikua zaidi ya (16) kutoka katika mikoa tofauti, kila kikundi kina (msomaji, mfasiri na haafidh), mashindano yaha yanaendeshwa chini ya kamati ya majaji walio bobea katika fani za Qur’an, hao ndio wanao husika na kuuliza maswali kwa kufuata utaratibu ulio pangwa na ndio walio tangaza washindi, mashindano yamefanyika siku (15) mfululizo jioni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: