Kufuatia kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s), shangwe na furaha zimetawala katika ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na imepambwa ndani na nje, kwa kuwekwa maua ya rangi tofauti na yenye muonekano mzuri ndani na nje ya ukumbi na katika korido zake, pamoja na juu ya dirisha la kaburi tukufu, hali kadhalika korido za Ataba zimepambwa na mabango yaliyo andikwa baadhi ya fadhila na sifa za Imamu Hassan Almujtaba (a.s), pamoja na kupamba ukuta wa haram tukufu kwa kuweka taa za rangi ndani na nje, yote hii ikiwa ni ishara ya kusherehekea kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s) ambaye alizaliwa siku kama ya kesho mwezi kumi na tano Ramadhani.
Atabatu Abbasiyya imesha andaa ratiba maalumu kwa ajili ya kuadhimisha tukio hili tukufu na kuiingiza katika ratiba zake za mwezi wa Ramadhani, ambapo kutakua na mihadhara ya dini ratiba za kitamaduni na kielimu, kama vile kufanyika kwa kongamano la Kariimu Ahlulbait Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika mji wa Hilla mwezi kumi na nne na litadumu siku tatu litakalo kua na vipengele vingi, ambalo ni hafla kubwa zaidi ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s).
Kumbuka kua Imamu Hassan bun Amirulmu-uminina Ali Bun Abu Twalib (a.s) alizaliwa mwaka wa tatu hijiriyya usiku wa Juma nne, nusu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani –kauli mashuhuri- Malaika Jibrilu alikuja kwa Mtume akamuambia: Hakika Mwenyezi Mungu anakutumia salamu na anakuambia: jina lake ni Hassan, akawa kaitwa jina hilo, kisha akafanyiwa hakika na akanyolewa nywele zake kisha Mtume akatoa sadaka ya fedha kwa uzito wa nywele hizo na akampa jina la kuniya la Baba Muhammad (Abuu Muhammad).