Usiku wa mwezi kumi na tano Ramadhani dunia iliangaziwa na nuru ya kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Hassan Almujtaba (a.s)…

Maoni katika picha
Katika nyumba alizo amrisha Mwenyezi Mungu zijengwe na litajwe ndani jina lake ndani yake, imechomoza nuru katika ulimwengu wa kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu kwa kupitia nuru hiyo aliuinia uislamu, na akakazia swala la imani, na akaweka maelewano baina ya makundi mawili makubwa naye ni mjukuu wa Mtume Muhammad Imamu Hassan Almujtaba (a.s), ambaye usiku wa mwezi kumi na tano katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ndio siku aliyo zaliwa.

Ibun Baabawaihi amepokea kwa sanadi zinazo kubalika kutoka kwa Imamu Zainul-Aabidina (a.s) kua, alisema (a.s): Fatuma alipo jufungua Hassan (a.s) Alimuambia Ali mpe jina, Akasema: Siwezi kumtangulia Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kumpa jina, akaja Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), akapelekewa mtoto akiwa kafungwa katika kitambaa cha njano, Akasema: Sikukukatazeni kumfunga katika kitambaa cha njano? Kisha wakambadilisha na kumfunga katika kitambaa cheupe, akamuuliza Ali (a.s) Je umempa jina? Akasema: Siwezi kukutangulia kumpa jina, Akasema (s.a.w.w): na mimi siwezi kutangulia Mwenyezi Mungu mtukufu kumpa jina, Mwenyezi Mungu akamuambia Jibrilu kua katika nyuma ya Muhammadi kazaliwa mtoto nenda kampe salamu zangu na umpongeze, halafu umuambie: Hakika Ali kwako ni sawa na Haruna kwa Mussa, mpe jina la mtoto wa Haruna, Jibrilu (a.s) akaja kwa Mtume (s.a.w.w) akampa salam na pongezi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasema: Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu anakuamrisha umpe jina la mtoto wa Haruna, akasema, alikua anaitwa nani? Akasema: Shabbir, Akasema kwa lugha ya Kiarabu, mwite Hassan, ndio akaitwa Hassan.

Alipo zaliwa Hussein (a.s) Mwenyezi Mungu alimuambia Jibrilu (a.s), Hakika katika nyumba ya Muhammad kazaliwa mtoto, nenda ukampongeze na umwambie: Hakika Ali kwako ni sawa ha Haruna kwa Mussa mwite jina la mtoto wa Haruna, akasema: Jibrilu (a.s) akaenda kwa Mtume (s.a.w.w) akampa pongezi kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, kisha akasema: Hakika Ali kwako ni sawa na Haruna kwa Mussa, mwite jina la mtoto wa Haruna, Akasema: jina lake nani? Akasema: Shabiir, kwa lugha ya kiarabu ni Hussein, Akaitwa Hussein.

Shekh mtukufu Ali bun Issa Arbaliy (r.a) ameandika katika kitabu cha Kashfu Ghummah kua: Hassan bun Ali (a.s) alikua na weupe unaomili katika wekundu, mwenye macho mazuri, mashavu yake yamekaa vizuri, mwili wake umejazia vizuri, mwenye ndevu nyingi zilizo kaa vizuri, shingo lake zuri, viungo vyake vina nguvu (msuli), alikua na kimo cha kati na kati sio mrefu wala sio mfupi, alikua na sura nzuri sana, alikua na nywele nyingi na mwili mzuri.

Imepokelewa kutoka kwa Imamu Ali (a.s) alisema: (Hassan amefanana mno na Mtume (s.w.w.w) kifua na kichwa, na Hussein amefanana mno na Mtume kuanzia kifuani kushuka chini).

Mtume (s.a.w.w) aliona kua mjukuu wake Hassan (a.s), anafanana naye katika tabia, ni kopi yake katika utukufu wa nafsi, ataongoza umma wake baada yake katika njia ya haki, alibaini (s.a.w.w) kupitia elimu ya ghaibu kua kila jambo lenye umuhimu mkubwa atalifanya katika maisha yake, alimpa nafasi kubwa katika roho yake tukufu, alimuonyesha mapenzi ya hali ya juu, kuanzia kuzaliwa kwake, kulelewa kwake kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: