Kwa usimamizi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya: Kuanza kwa kongamano kubwa la kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s)…

Maoni katika picha
Katika usiku unaogawa mwezi mtukufu wa Ramadhani, unaoshangiliwa kila upande na watu wanapongezana katika usiku huo, kwa sababu mwezi wa Aali Muhammad watukufu (a.s) umefika katika kilele chake, hakika ni kuchomoza kwa Hassan Zakiyyu (a.s) mjukuu wa Mtume mtukufu (s.a.w.w), imeenea shangwe na furaha kwa kuzaliwa nuru nyingine miongoni mwa nuru za nyumba ya Muhammad.

Mwaka wa kumi na moja mfululizo chini ya usimamizi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, jioni ya jana (14 Ramadhani 1439h) sawa na (30 Mei 2018m) lilizinduliwa kongamano la kitamaduni la kuadhimisha kuzaliwa kwa Kariim Aalulbait (a.s) linalo simamiwa na watu wa Hilla mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hassan –a.s- ni muokozi wa waislamu na mfichuaji wa uovu wa wanafiki), kwa kushirikiana na ofisi ya wakfu shia ya mkoa, kwa ajili ya kuhuisha na kuadhimisha kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume Imamu Hassan (a.s).

Hafla ya ufunguzi ilifanyika katika bustani ya muujiza wa kurudisha jua (Radu Shamsi) wa Imamu Ali (a.s) katikati ya mji wa Hilla, ilipata mahudhurio makubwa ya viongozi mbalimbali na wageni walio wakilisha vitengo tofauti vya kisekula na kidini pamoja na vyombo vya habari na wengineo, ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya watu wa Hilla na wawakilishi wa Ataba mbalimbali na Mazaru tofauti.

Baada ya kusoma Qur’an ya ufunguzi na kusoma surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq ambao kutokana na damu zao tukufu pamoja na kujitolea kwao tumefanikiwa kufanya kongamano hili, wahudhuriaji walielekea katika shughuli ya kupandisha bendera ya Imamu Hassan (a.s) na kuifanya ipepee katika mazaru hiyo na kukutana na nyoyo za wapenzi wake wakiwa wanaangalia inavyo pepea angani.

Ukafuata ujumbe wa watu wa Hilla ulio wasilishwa kwa niaba yao na mjumbe wa kamati ya maandalizi Muhandisi Haasan Alhilliy.

Hali kadhalika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya zilikua na ujumbe rasmi ulio wasilishwa na Ustadh Maitham Zaidi.

Hafla ya ufunguzi ilikua na vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na igizo liitwalo (Kawaida ya ushindi) lililo tungwa na kutolewa na Ustadh Muhammad Hussein Habibu kutoka katika kitivo cha sanaa katika chuo kikuu cha Baabil, aliweza kuwatumia vizuri watalamu wake katika igizo hilo, lililo jaa khutuba na mawaidha ya Imamu Hassan (a.s) na kuowanisha na mazingira ya sasa wanayo ishi Wairaq na waliyo ishi kipindi cha vita ya kukomboa ardhi yao tukufu.

Pia kulikua na kaswida zilizo imbwa na mshairi wa Kibaharain Ustadh Hussein Aabid aliye burudisha masikio na nyoyo za wahudhuriaji kwa vipande murua vya mashairi, alianza na qaswida isemayo (kutokana na wito ulioitikiwa kwa nguvu na kujiamini) iliyo kua inaashiria fatwa ya Marjaa dini mkuu ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu, na kaswida nyingine ilikua inamuhusu muhusika wa kongamano hili iliyo kua inasema: (Amechomoza mgeni wako hakika ulimwengu umesha wasili).

Pia kulikua na kaswida za kimashairi zilizo somwa katika vipindi vya mapumziko na kikosi cha kimataifa cha kaswida za kiislamu kilicho chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu, na mwisho mwimbaji mashuhuri Hamidi Twawirijawi alisoma beti zilizo onyesha mapenzi ya hali ya juu kwa Imamu Hassan (a.s).

Kisha wahudhuriaji wakaelekea katika ufunguzi wa maonyesho ya kazi za mikono zinazo fanywa na kikundi cha vijana wa Hamza katika mkoa wa Baabil.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: