Bendera ya mkarimu wa Ahlulbait (a.s) inapepea katika anga ya Hilla katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake…

Maoni katika picha
Kundi la wapenzi wa mjukuu wa Mtume lanyoosha mikono juu, wakiomba rehma za Mola wao, hakika hii ni mikono ya watu wenye mapenzi ya kweli kwa Muhammad na watu wa nyumbani kwake watakatifu (a.s), inayo nyooshwa katika anga la Hilla kwa kuonyesha mapenzi yao, hakika ni bendera ya Kariim Ahlulbait watukufu (a.s) walio kutana na matatizo mengi.

Ewe Mujtaba! Una bendera katika kila moyo, mapenzi ya dhati na amani, na katika kila jicho uaminifu, ewe uliye wapa nguvu waumini na muokozi wa washika dini, hii hapa bendera ya ushindi ambayo ni ishara ya kufuata mwenendo wenu mtukufu na njia yenu iliyo nyooka inapandishwa juu kuwaangamiza wanafiki na madhalimu.

Imekua desturi kila mwaka shughuli za kongamano la kitamaduni la kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s) huzinduliwa kwa kupandishwa bendera ya kijani iliyo andikwa: (Ewe Kariim wa Aalul Bait), leo hii inapandishwa katika mazaru ya muujiza wa kurudisha jua (Radu Shamsi) wa Imamu Ali (a.s) na kupepea katika anga la Hilla.

Katika shughuli hii tukufu wameshiriki watu wa Hilla na wageni wa kongamano ambao ni viongozi wa dini na wasiokua wa dini kutoka ndani na nje ya mkoa wa Baabil.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: