Kwa picha: Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) watoa pongezi kwake katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa ndugu yake Imamu Hassan Almujtaba (a.s)…

Maoni katika picha
Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wametoa pongezi kwake kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa ndugu yake Kariim Aalul Bait (a.s), katika shughuli ambayo hufanywa kila wiki siku ya Juma Tatu na Alkhamisi, Alkamisi hii imesadifu sherehe za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kote duniani, wanaimba na kusoma mashairi yanayo onyesha mapenzi yao kwa Imamu Hussan (a.s), nyumba ya Muhammad (s.a.w.w) ilijaa furaha katika siku kama ya leo mwezi kumi na tano Ramadhani.

Kumbuka kua Imamu Hassan mtoto wa Kiongozi wa Waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) alizaliwa mwaka wa tatu Hijiriyya katika usiku wa Juma Nne, mwezi kumi na tano Ramadhani –kwa kauli mashuhuri- alishuka Malaika Jibrilu kwa Mtume (s.a.w.w) akamwambia: Hakika Mwenyezi Mungu anakutolea salamu salamu na anakuambia: Mwite Hassan, Akapewa jina la Hassan, kisha akafanyiwa hakika na akanyolewa nywele na kutolewa sadaka ya fedha kwa uzito wa nywele zake na akapewa jina la kuniyya la baba Muhammad (Abu Muhammad)
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: