Kumbukumbu za mwezi wa Ramadhani: Kuondoka kwa balozi wa Imamu Hussein (a.s) Muslim bun Aqiil kwenda katika mji wa Kufa…

Maoni katika picha
Siku kama hizi ndani ya mwezi wa Ramadhani ni siku za utangulizi wa muhanga wa Imamu Hussein (a.s), mwezi kumi na tano Ramadhani Imamu Hussein (a.s) alimtuma balozi wake na mtu muaminifu kwake mtoto wa Ammi yake Muslim bun Aqiil (a.s) kwenda katika mji wa Kufa, kwani alikua ni mtu mwenye hekima, shujaa na ikhlasi, akamwagiza aende akaangalie mazingira, na amuelezee hali halisi ili aweze kufanya maamuzi sahihi.

Baada ya kupokea barua nyingi kutoka kwa watu wa Kufa, wakimuomba na kumhimiza aende kuwaokoa na dhulma za utawala wa Umawiyya, baadhi ya barua hizo zilikua zinambebesha majukumu mbele ya Mwenyezi Mungu na katika umma wa kiislamu iwapo atachelewa kwenda. Ndipo Imamu akaona kabla ya kufanya maamuzi yoyote amtume balozi wake kwao atakaye mpa taarifa kamili kuhusu mazingira yao na ukweli wao, akiwakuta wana nia za kweli na msimamo imara, achukue kiapo cha utiifu kwao, kisha yeye ndio aende baada ya hapo, alimteua mtu mwaminifu kwake na mkubwa ki-umri katika watu wa nyumba ya Mtume (a.s) ambaye ni Muslim bun Aqiil, naye alikubali jukumu hilo bila kinyongo, akampa barua isemayo:

(kutoka kwa Hussein bun Ali kwenda kwa kila atakaye fikiwa na barua hii miongoni mwa wapenzi wake na wafuasi wake katika mji wa Kufa:

Asalamu alaikum, Amma ba’ad: Zimenijia barua zenu, na nimefahamu mliyo taja ndani ya barua hizo, ambayo ni kunitaka nije kwenu, mimi namtuma kwenu ndugu yangu na mtoto wa Ammi yangu na mtu muaminifu kwangu katika watu wa familia yangu Muslim bun Aqiil, ili aniambie uhalisia wa jambo lenu, na ataniandikia atakacho kibaini katika mkutano wenu, ikiwa hali ipo kama zinavyo sema barua zenu, nitafanya haraka kuja kwenu Inshallah, wasalam.

Muslim alichukua barua na akaondoka Maka usiku wa mwezi kumi na tano Ramadhani akielekea Kufa kwa kupitia Madina, alipo fika Madina akaswali katika msikiti wa Mtume (s.a.w.w), na akazunguka kaburi lake kisha akawaaga ndugu zake na maswahaba zake, ilikua ni kuwaaga kwa mara ya mwisho, akaondoka kuelekea Iraq, akaajiri vijana wawili wakumuelekeza njia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: