Baada ya siku sita za shangwe na furaha walizo ishi wapenzi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), jioni ya jana Juma Mosi (16 Ramadhani 1439h) sawa na (1 Juni 2018m) ndani ya ukumbi wa wakfu shia katika mkoa wa Baabil, ilifanyika hafla ya kufunga kongamano la kumi na moja la kuadhimisha kuzaliwa kwa Mkarimu wa Ahlulbait (a.s), linalo simamiwa na kamati kuu ya miradi ya Hilla mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) chini ya ulezi wa Ataba mbili Tukufu Husseiniyya na Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hassan –a.s- ni muokozi wa waislamu wa mfichuaji wa uwovu wa wanafiki).
Hafla ya kufunga kongamano ilikua na vikao viwili vya kitafiti na lilihudhuriwa na ugeni rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kundi kubwa la Masayyid na Mashekh na jopo la walimu wa kisekula kutoka katika vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya mji wa Hilla.
Baada ya kusomwa Qur’an tukufu ya ufunguzi na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kilifanyika kikao cha kwanza cha uwasilishaji wa mada ya kitafiti iliyo wasilishwa na mtafiti wa kiislamu Dokta Hassan Issa Alhakim, utafiti wake ulikua unasema: (Shubuha zilizo tolewa kuhusu Imamu Hassan –a.s- na njia za kuzijibu), alielezea mambo kadhaa yaliyo onyesha kudhulumiwa kwa Imamu Hassani (a.s), kwa kuzusha hadithi ambazo sio za kweli zilizo andikwa na wapotoshaji wa historia, na akaelezea baadhi ya matukio kuhusu Imamu Almujtaba (a.s), akafafanua matukio sahihi na yasiyo kua sahihi, akalinganisha baadhi ya matukio hayo na hadithi zenye sanadi na visomo tofauti.
Kikao kingine cha kiutafiti kilifanyika baada ya swala ya Isha, ambapo mtafiti Sayyid Ali Muhammad Hussein Twabatwabai aliwasilishwa utafiti wake ulio kua unasema: (Nafasi ya Imamu Hussan katika uhai wa kisiasa na wa mambo mengine), akaelezea mambo kadhaa, miongoni mwa mambo hayo ni suluhu ya Imamu Hassan (a.s) pamoja na Muawiya, na nafasi yake ya kujenga maelewano katika tukio hilo na jinsi alivyo linda uislamu na waislamu, pamoja na mambo mengine yanayo husiana na tukio hilo, akalinganisha tukio hilo na muhanga wa Imamu Hussein (a.s).
Vikao hivyo vya kitafiti vilikua na michango mingi ya kielimu pamoja na maswali mengi, watafiti walijibu maswali na kufafanua sehemu zilizo hitaji ufafanuzi zaidi.
Mwisho kabisa ulifuata ufungaji wa kongamano hilo kwa kuwasilishwa ujumbe wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, ulio wasilishwa na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Abbasi Didah, ambaye aliwasilisha salamu za viongozi wakuu wa kisheria wa Ataba mbili tukufu kwa wasimamizi wa kongamano hili, akaomba kuendeleza juhudi hizi na akapongeza kazi nzuri iliyo fanyika kuhakikisha kongamano la kumi na moja linafanyika, awamu hii ambayo inazingatiwa kua inakamilisha mazuri ya awamu zilizo tangulia na inafungua milango ya mazuri katika awamu zijazo, awamu hii ilikua na ratiba iliyo dumu siku sita, siku tatu za mwanzo ratiba yake iliitwa pembezoni mwa kongamano, ambayo ilihusisha kutoa zawadi kwa vyombo vya habari, hafla ya kumpongeza Alamah ibun Idrisa Alhilliy pamoja na hafla ya kutoa zawadi kwa familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi, iliyo simamiwa na Atabatu Kadhimiyya tukufu, na ratiba ya baada ya ufunguzi rasmi ilihusu, uwasilishaji wa ujumbe mbalimbali, usomaji wa kaswida na mashairi na kuhitimishwa na vikao vya kitafiti, juhudi hiyo ni kubwa na inastahiki pongezi, hongera sana kwa wakazi wa mkoa huu uliokua kitovu cha elimu na wanachuoni, na ukasifika kua ni mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s).
Hafla hii ilipambwa na kaswida za kimashairi pamoja na kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la Imamu Hassan Almujtaba (a.s) lililo fanyika kabwa ya mwezi mmoja, na mwisho kabisa wageni wa kongamano walio wasilisha mada za kiutafiti, wana habari, kamati ya maandalizi ya kongamano hili na kila aliye changia mafanikio ya kongamano hili wakapewa midani.