Kumbukumbu za mwezi wa Ramadhani: Vita ya Badri na utukufu wa Amirul Mu-uminina (a.s) (wa kusalimiwa na Malaika) elfu tatu…

Maoni katika picha
Siku ya tarehe kumi na saba ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ina tukio kubwa kwa waislamu wote, ni siku ya kumbukumbu ya vita ya Badri, ambayo ni vita ya kwanza baina ya waislamu na makafiri wa kikuraishi, pia vita hii ni miongoni mwa vita mashuhuri zaidi iliyo ongozwa na Mtume (s.a.w.w) dhidi ya makafiri, ina nafasi kubwa katika historia ya kiislamu ukilinganisha na vita zingine, maswahaba walio shiriki katika vita hii wamepata heshima kubwa na utukufu wapekee kabisa, historia imeelezea ushujaa wao kwa utukufu mkubwa.

Baada ya Mtume (s.a.w.w) kufahamu idadi ya wapiganaji wa makuraishi na viongozi wao… aliwaambia wapiganaji wake walio kua wachache na wenye siraha duni za kivita ukilinganisha na makuraishi, Mtume (s.a.w.w) akasema: (Hawa watu wa Maka wamekujieni na wapiganaji wao hodari)… Vita ikaanza, Ali (a.s) akaingia katika uwanja wa mapambano, majeshi mawili yakaanza kupigana kwa mishale na majambia… Mwenyezi Mungu (akatoa amri Malaika wakaingia vitani kuwasaidia waislamu)… wailamu wakawashinda washirikina… na ushindi wa waislamu ilikua ni ahadi ya kweli ya Mwenyezi Mungu, waumini wakajaa imani zaidi… wakawauwa washirikina kwa jambia zao, upanga wa Dhulfiqaar uliua nusu ya washirikina wote walio uawa katika vita hiyo… Makuraishi waliumizwa sana kwa kuuawa kwao lakini wakaficha machungu yao mbele ya Mtume na maswahaba wake…

Waumini walifurahi sana kwa ushindi huo, na watu wakaanza kuingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi, hivi ndio waumini walivyo pata nguvu kwa kupewa nusra na Mwenyezi Mungu, habari zikaenea katika nchi za uarabuni na maeneo yanayo zizunguka… ikawaka nyota mpya ya uongozi katika nchi za uarabuni, kila mtu akaanza kulijadili taifa hili change, mji wa Madina ukawa makao makuu ya umma wa kiislamu, alhamdu lillahi kwa ushindi huo, na Mwenyezi Mungu ndio mtegemewa kwa kila kitu.

Kuhusu usiku wa vita kuna riwaya nyingi, inasemekana Mtume (s.a.w.w) aliwaambia maswahaba wake katika usiku wa Badri: Nani miongoni mwenu anaweza kwenda kisimani kutuletea maji ya kunywa? Wakakaa kimya hakuna aliye weza jambo hilo, kiongozi wa waislamu (a.s) akachukua kiriba na akaenda kuchota maji, ulikua usiku wa giza wenye baridi na upepo mkali, alipo fika kisimani hakupata ndoo ya kuchotea maji, kisima kilikua kirefu na kina giza nene, akaingia ndani ya kisima, akachota maji na kujaza kiriba chake kisha akatoka na akaanza kurudi kwa Mtume (s.a.w.w), ukaja upepo mkali, akakaa hadi ulipo tulia, akasimama na kuendelea na safari, mara ukaja tena upepo mkali kama wa mara ya kwanza, akakaa tena juu ya ardhi hadi ulipo tulia, alipo taka kuendelea na safari ukaja tema kwa mara ya tatu, akakaa tena hadi ulipo tulia, akasimama na kwenda hadi kwa Mtume (s.a.w.w), Mtume akamuuliza: Ewe baba Hassan kwa nini umechelewa? Akasema: (a.s): nipekumbwa na upepo mkali mara tatu, nikakaa hadi utulie, Mtume (s.a.w.w) akasema: Je unaufahamu upepo huo ewe Ali? Akasema (a.s): Hapana.

Akasema (s.a.w.w) upepo wa kwanza alikua ni Jibrilu akiwa na malaika elfu moja, alikutolea salamu na malaika wote wakakutolea salamu, na wa pili alikua ni Mikaeli, akiwa na malaika elfu moja, alikutolea salamu na malaika wakakutolea salamu, na wa tatu, alikua ni Israfiil akiwa na malaika elfu moja, alikutolea salamu na malaika wote wakakutolea salamu, wote wamekuja kutusaidia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: