Ibada za siku za Lailatul Qadri zipo za aina mbili: aina ya kwanza hufanywa katika siku zote tatu za Lailatul Qadri, (mwezi 19, 21 na 23), aina ya pili ni ibada maalumu kwa ajili ya siku hizo tu. Sayyid ibun Twausi ameandika katika kitabu cha Iqbaal: kutoka kwa Imamu Baaqir (a.s): (Atakaye fanya ibada katika usiku wa Lailatul Qadri atasamehewa dhambi zake hata kama zikiwa nyingi kama idadi ya nyota za mbinguni na nzito kama milima na zinaujazo kama wa bahari).
Hivyo inatakiwa kuzingatia sana, asiye jali siku hizi hawezi kupata utukufu wa Lailatul Qadri, mwanadamu anapo zijali na kuzitukuza siku hizo hupata tunu fulani kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya Lailatul Qadri zijazo. Ibada za siku hizi zimegawanyika sehemu mbili:
Ibada za siku za Lailatul Qadri
- 1- Kuoga, ni bora uoge wakati wa kuzama jua ili uswali Magharibi na Isha baada ya kuoga kwako.
- 2- Swala ya rakaa mbili, katika kila rakaa soma Alhamdu na surat Tauhidi mara saba, baada ya kumaliza swala useme: (Astaghfiru llaha wa Atuubu ilaihi) mara sabini, utapata thawabu nyingi sana.
- 3- Dua ya kufungua msahafu, katika siku tatu za Lailatul Qadri fungua msahafu na uuweke mbele yako kisha useme: (Allahumma inni As-aluka bikitaabika-munzal, wa maa fiihi, wa fiihi ismukal-akbaru, wa asmaaukal husna wa maa yukhafu wa yurja an taj’alani min utqaaika mina nnaar) kisha uombe haja zako.
- 4- Dua ya kuweka misahafu kichwani na kutawasal kwa Mwenyezi Mungu kupitia misahafu hiyo. Chukua msahafu uufunguwe na kuuweka kichwani kwako na useme: (Allahumma bihaqi hadhal Qur’an, wa bihaqi man arsaltahu bihi, wa bihaqi kullu mu-umin madahtahu fiihi, wa bihaqika alaihim, falaa ahada a’arafa bihaqika minka, bika yaa Allah, mara kumi. kisha useme: Bi Muhammad, mara kuni. Bi Ali, mara kumi. Bi Fatuma, mara kumi. Bil Hassan, mara kumi. Bil Hussein, mara kumi. Bi Ali bun Hussein, mara kumi. Bi Muhammad bun Ali, mara kumi. Bi Jafari bun Muhammad, mara kumi. Bi Mussa bun Jafari, mara kumi. Bi Ali bun Mussa, mara kumi. Bi Muhammad bun Ali, mara kumi. Bi Ali bun Muhammad, mara kumi. Bil Hassan bun Ali, mara kumi. Bil Hujjah, mara kumi. Kisha uombe haja yako, imepokewa katika hadithi kua dua zako zitajibiwa na utakidhiwa haja zako.
- 5- Ziara maalumu ya Imamu Hussein (a.s).
- 6- Kuhuisha usiku wa siku hizo tatu kwa kufanya ibada.
- 7- Kuswali rakaa (100), hakika swala hiyo inafadhila nyingi sana, ni vizuri kusoma Alhamdu na surat Tauhidi (Qul-huwallahu Ahad) mara kumi, katika kila rakaa.
Ibada maalumu za usiku:
- 1- Sema: Astaghfirullaha Rabbii wa atuubu ilaika. Mara (100).
- 2- Sema: Allahumma l’an qatlata Amiril-mu-uminina. Mara (100).
- 3- Soma dua isemayo: (Allahumma lakal-hamdu ala maa wahabta lii min itwiwaai maa twawaita min shaharii, wa innaka lam tujin fiihi ajalii, wa lam taqtwaa umrii, wa lam tubilnii bi mardhi yadhurunii ilaa tarki swiyaam, walaa bisafarin yahillu lii fiihil-iftwaaru, fa-anaa asuumuhu fii kifayatika wawiqaayatika, atwiiu amraka, waiqtaatu rizqika, wa arjuu wa uammilu tajaauzaka, fa-atmim Allahumma alayya fii dhalika ni’imataka, wajzil fiihi minnataka, waslukhhu annii bikamali swiyami watamhiswil-aathaami, wabalighnii aakhiratu bi khaatimati khairin wa khairahu, ya ajwadal mas-uliina, wa yaa asmahal waahibiina, wa swala llahu alaa Muhammad wa Aalihi twaahiriin).
- 4- Soma dua isemayo: (Yaa dha lladhii kaana qabla kulla shai-in, thumma khalaqa kulla shai-in, thumma yabqa wa yafna kulla shai-in, yaa dhaa lladhii laisa fii samaawaatil-ulaa, walaa fil-aradhiina sulfa, walaa fauqahunna walaa bainahunna walaa tahta hunna ilaahun yu’ubadu ghairuhu, lakal-hamdu hamdan laa yaqdiru alaa ihswaaihi illaa anta, faswalli alaa Muhammad wa Aali Muhammad, swalaatan laa yaqdir alaa ihswaaihi ilaa anta).
- 5- Kusoma dua isemayo: (Allahumma ij’al fimaa taqdhi wa yuqadaru minal-amril mahtuumi, wa fimaa tufaruqu minal-amril hakiimi fii lailatil Qadri, wa fil qadhwaai lladhii laa yuraddu walaa yubaddal, an-taktubanii minal hujjaaji baitikal haraami, almabruuri hajjuhum, almashkuuri sa’ayihim, almaghfuri dhunuubuhum, almukaffar anhum sayyiaatihim, waj’al fiimaa taqdhi wa tuqaddiru, an tatwiila umrii, watuwassi’a alayya fii rizqii wa taf’al bii kadha wa kadha)
- 6- kusoma dua isemayo: (Allahumma innii amsaitu laka abdan daakhilan laa amliku linafsi dhwaran walaa naf’aa, walaa usrifu anha suuan, ushhidu bidhaalika alaa nafsii, wa-a’tarifu laka bidhwa’afi quwwatii, wa qillata hiilatii, faswalli alaa Muhammad wa aali Muhammad, wa-anjizlii maa wa’adtanii, wa jami’al mu-uminina wal mu-minaat minal maghfirat fii hadhihi llailah, watmim alayya maa a’atwaitanii, walaa aaisan min ijaabatika, wa-in abtwa-ata annii, fii saraaa kuntu au dhwaraa-a, au shiddatin au rakhaa-in, au aafiyatin au balaain, au bu-usin au na’amaa-a innaka samiiu du’aa).
- 7- dua ya mwisho katika usiku huu inatoka kwa Mtume (s.a.w.w) inasema: (Subhaana man laa yamuutu, subhaana man laa yazuulu mulkuhu, subhaana man laa takhfa alaihi khaafiyah, subhaana man laa tasqutu waraqata illaa bi’ilmihi, walaa habbatin fii dhulumaatil ardhi walaa ratbin walaa yaabisin illaa fii kitaabin mubiin, illaa bi’ilmihi wa biqudratihi fasubhaanahu subhaanahu, subhaanahu subhaanahu, subhaanahu subhaanahu, maa a’adhama sha-anahu, wa ajalla sultwaanahu, Allahumma swali alaa Muhammad wa aalihi, waj’alnaa min utaqaa-ika, wa suadaai khalqika bimaghfiratika innaka antal-ghafuuru rahiimu).