Shule za AL-Ameed zapata ufaulu mkubwa katika matokeo ya mitihani ya wizara ya shule za msingi…

Maoni katika picha
Kama sehemu ya muendelezo wa mafanikio yaliyo patikana, shule za Al-Ameed zilizo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zimepata ufaulu mkubwa unao zifanya kua shule maalumu. Wizara imetoa matokeo ya mitihani ya shule za msingi ya mwaka (2017 – 2018) katika mkoa mtukufu wa Karbala.

Katika taarifa iliyo tolewa na kitengo hicho kwa mtandao wa kimataifa Alkafeel inasema kiwango cha ufaulu kilikua kama ifuatavyo:

  • 1- Shule ya msingi ya wasichana Al-Ameed (100%).
  • 2- Shule ya msingi ya wasichana Nurul-Abbasi (a.s) (100%).
  • 3- Shule ya msingi ya wasichana Alqamar (100%).
  • 4- Shule ya msingi ya wavulana Al-Ameed (100%).
  • 5- Shule ya msingi ya Sayyidul-Maa (95%).
  • 6- Shule ya msingi ya wavulana Nurul-Abbasi (91%).

Wametoa pongezi kwa wanafunzi na walimu wao kwa ufaulu huo mkubwa, ambao ni matunda ya juhudi zao katika masomo, pia wametoa pongezi kwa uongozi wa shule na watalamu wao wa malezi na elimu kwa juhudi kubwa zilizo wezesha shule zao kupata kiwango kikubwa cha ufaulu, kwani washindi hufanya juhudi katika masomo kwanza, na ushindi hua ni matokeo ya juhudi zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: