Atabatu Abbasiyya tukufu yajiandaa kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Ali (a.s) na siku za Lailatul Qadri…

Maoni katika picha
Ratiba iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya mwezi wa Ramadhani inahusisha vipengele vingi vya kuhuisha matukio mbalimbali, likiwemo tukio la kumbukumbu ya kifo cha Imamu Ali (a.s) ambalo huendana na kuhuisha siku tukufu za Lailatul Qadri.

Ratiba hiyo inaaza leo na kesho ambayo ni siku aliyo jeruhiwa Imamu Ali (a.s) na siku ya Lailatul Qadri ya kwanza, na itaendelea hadi tarehe ishirini na tatu Ramadhani tukufu.

Atabatu Abbasiyya itashuhudia harakati mbalimbali zinazo endana na uhuishaji wa siku hizi tukufu, itatumia uwezo wake wote kuhakikisha inaandaa mazingira bora ya kufanya ziara na kusoma dua.

Hali kadhalika mihadhara na harakati za kidini zitajikita katika kuelezea utukufu wa siku hizi na matukio yake, pamoja na kuandaa tim ya watangazaji watakao rusha matukio yote moja kwa moja kupitia masafa ya bure watakayo itoa kwa vyombo vya habari.

Kuhusu siku ya kifo cha Imamu Ali (a.s) yatafanyika maombolezo ya aina mbalimbali, kutakua na majlisi ya kuomboleza ndani ya Atabatu Abbasiyya, kutakua na matembezi ya Maukibu ya Ataba mbili tukufu, pia tuta shiriki kuhuisha ibada ya ziara katika malalo ya Imamu Ali (a.s) katika mji wa Najafu, na tutajipanga kupokea Mawakibu za waombolezaji wanao kuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: