Katika kumbukumbu za Ramadhani: Usiku wa kumi na tisa wa Ramadhani alijeruhiwa Imamu Ali (a.s) ni siku ya huzuni kubwa baada ya siku aliyo kufa Mtume (s.a.w.w)…

Maoni katika picha
Mwambie ibun Muljim, umevunja dini na uislamu una nguzo zake.

Umeua mmbora wa wanaotembea kwa miguu na mbora wa watu katika uislamu na imani, mwezi wa Ramadhani wa mwaka wa arubaini hijiriyya, unatukio lenye kuumiza sana kwa waislamu baada ya kumkosa mtume wao (s.a.w.w), tukio hilo lilipangwa na muovu wa waovu Abdurahmaani bun Muljim Almuradi (laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) katika mji wa Maka akiwa na kundi la maswahaba wake makhawaariji.

Imepokewa kua, Ulipo ingia mwezi wa Ramadhani Amirul Mu-minina (a.s) alikua anafuturu siku moja kwa Hassan na siku nyingine kwa Abdullahi bun Abbasi, alikua hazidisha tonge tatu, siku moja akaulizwa: Una tatizo gani mbona hauli? Akasema: Napenda amri ya Mwenyezi Mungu inijie tumbo langu likiwa tupu, baada ya hapo alikaa siku moja au mbili akajeruhiwa.

Imepokewa kua Imamu Amirul Mu-uminina (a.s) alipo taka kuondoka nyumbani kwake siku aliyo jeruhiwa, baada ya simama katika uwanja wa nyumba alizungukwa na bata maji wakawa wanalia mbele ya uso wake, wakataka kuwafukuza, akasema (a.s): Waacheni hakika hiki ni kilio cha bata maji kitafuata kilio cha watu…

Sharifu Ridha (r.a) anasema: Ali (a.s) alikesha katika usiku ambao asubuhi yake alipigwa panga, akasema: Mimi nitauawa, kama ikifika asubuhi na pakiadhiniwa nitatembea kidogo, binti yake Zainabu akasema: Ewe Kiongozi wa Waumini mwambie Ju’uda aswalishe watu, Akasema: Hauwezi kukimbia (amri ya Mwenyezi Mungu) kisha akatoka.

Hadithi nyingine, inasema: Imamu (a.s) hakulala katika usiku alio jeruhiwa, alikua anaangalia sana mbinguni, na anasema: Wallahi sijawahi kudanganya wala kudanganywa, hakika huu ni usiku niliyo ahidiwa, ilipo fika asubuhi akafunga msuli wake huku anasema:

Nakaza mkanda kwa kujiandaa na kifo hakika kifo kitanikuta.

Wala usiogope kufa unapo fika muda wake.

Imamu (a.s) akatoka nyumbani kwake na akaenda kuswalisha watu, alipo kua katika sijida ndani ya mihrabu yake, maluuni ibun Muljim alimpiga kichwani kwa panga lenye sumu kali, Imamu (a.s) akasema: Nimefuzu kwa haki ya Mola wa Kaba. Sumu ikasambaa katika kichwa cha Imamu na ndani ya mwili wake, watu wote walio kua msikitini wakasambaa kumtafuta Maluuni ibun Muljim, wakainua siraha zao, ikawa inaonekana mikono tu iliyo shika siraha huku wakipiga kelele, Ibun Muljim alimpiga kwa uwoga na akakimbia.

Watu wakamzunguka Kiongozi wa Waumini (a.s) katika mihrabu yake huku akifunga jeraha na akiweka udongo kwenye jeraha, kisha akasoma aya isemayo: (Kutokana nayo (ardhi) tumekuumbeni, na humo tutakurejesheni, na kutoka humo tutakutoeni mara nyengine) kisha akasema (a.s): Imekuja amri ya Mwenyezi Mungu na kasema kweli Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).

Watu walipo sikia jambo hilo walitoka wakawa wanazunguka wala hawajui waendako kutokana na uchungu wa jambo hilo, wakamzunguka Kiongozi wa Waumini (a.s) huku anafunga kichwa chake kwa msuli wake, na damu inamtoka ikiwa imejaa usoni kwake na kwenye ndevu zake tukufu, huku anasema: Hili ndio alilo ahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kasema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Imamu Ali (a.s) hakuweza kusimama tena, akarudi nyuma akaswali akiwa amekaa huku akiendelea kufuta damu usoni na kwenye ndevu zake, na Imamu Hassan akatangulia mbele na kuswalisha watu, (baada ya swala) Hassan (a.s) akasema: umekatika mgongo (nguvu zimeniisha) ni jambo gumu kwangu kukuona (baba yangu) ukiwa katika hali hii, akafumbua macho yake akasema: Ewe mwanangu baba yako sina chakufanya baada ya leo, huyu hapa babu yako Muhammad na bibi yako Khadija na mama yako Fatuma Zaharaa na Hurul-ain wamekuja wanasubiri kuondoka kwa baba yako, tulia na upunguze kulia, hakika malaika sauti zao zimekua kubwa hadi mbinguni.

Kisha wakambeba Kiongozi wa Waumini hadi nyumbani, bibi Zainabu na Ummu Kulthum na wanafamilia wengine walikua wamesimama mlangoni wakimsubiri, walipo muona analetwa akiwa katika hali hiyo, waliangua vilio wakawa wanasema: Waa abataahu, Waa muswibataahu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: