Kwa picha: Ibada za usiku wa Lailatul Qadri wa kwanza na tukio la kujeruhiwa kwa Imamu Ali (a.s)…

Maoni katika picha
Mwenyezi Mungu mtukufu ameufadhilisha mwezi wa Ramadhani kushinda miezi mingine, na ameweka usiku wa Lailatul Qadri ambao ni usiku bora kushinda miezi elfu moja katika mwezi huu, ni mashuhuri kwamba usiku wa kumi na tisa wa mwezi huu ni miongoni mwa siku tukufu mno ambazo Mwenyezi Mungu anatwita kwake ili atufungulie milango ya toba na kunufaika na ukarimu wake kwa kupata msamaha wake na kutupa mambo mazuri yatakayo tunufaisha duniani na akhera.

Katika haram tukufu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na pembezoni mwake, kama kawaida ya waumini katika siku kama hii tukufu ya Lailatul Qadri ya kwanza, wamefurika waumini wanao fanya ibada mbalimbali imma kwa vikundi au mmoja mmoja, Atabatu Abbasiyya imeandaa idadi kubwa ya misahafu na vitabu vya dua, pamoja na kuandaa maeneo maalumu kwa ajili ya kufanya ibada ndani na nje ya haram tukufu kwa upande wa wanaume na wanawake.

Ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umejaa waumini wanao fanya ibada katika usiku huu mtukufu, wanao soma dua mbalimbali ikiwemo dua ya kunyanyua misahafu, tahajudi, kusoma Qur’an na nyeradi maalumu za usiku huu, wakiwa na matumaini ya kupata maghfira na kuepushwa na moto.

Sambamba na kukumbuka msiba mkubwa walio pata waislamu, ambao ni kifo cha Kiongozi wa Waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), kulikua na kipengele maalumu cha kutoa mihadhara ya kidini na kufanya majlisi za kuomboleza.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu katika ratiba yake ya mwezi wa Ramadhani, inakipengele maalumu cha (kukumbuka kifo cha Imamu Ali (a.s) pamoja na kuhuisha siku tukufu za Lailatul Qadri), kipengele cha utoaji wa mihadhara ya mwezi wa Ramadhani, inayo tolewa kila siku, hivi sasa mihadhara yote inazungumzia utukufu wa siku hizi na tukio la kujeruhiwa Kiongozi wa Waumini hadi kufa kwake kishahidi (a.s), kila siku zinafanyika majlisi za kuomboleza (matam) baada ya mihadhara, hali kadhalika yamefanyika maandalizi ya kutosha yanayo wawezesha mazuwaru watukufu kufanya ibada kwa utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: