Ramadhani katika kumbukumbu ya Karbala: Watu wa Karbala na kumbukumbu ya kifo cha Imamu Ali (a.s)…

Maoni katika picha
Unapo fika usiku wa kumi na tisa Ramadhani utaona nyumba za Karbala zimewekwa mapambo meusi, na huzuni hudhihirika katika nyuso zao, utawaona wakielekea katika haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) kumpa pole na kumliwaza bibi Zainabu (a.s) kwa msiba huu mkubwa, huwenda Mwenyezi Mungu anaweza kukubali taazia yao, kwa nini asikubali wakati huu ni usiku aliotoka Kiongozi wa Waumini Ali bun Abuu Twalib (a.s), siku ambayo watu wa Karbala hurudia kufanya vikao vya kuomboleza, haiwezi kufika Alfajiri bila kusikia sauti katika minara zikisema (Wallahi nguzo za uongofu zimevunjika).

Ustadh Khabbaaz kiongozi wa idara ya habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu anatukumbusha namna walivyo kua wakihuisha siku hizi watu wa Karbala, Ali Khabbaaz anasema: “Huzuni ilikua inaenea katika nyumba za Karbala katika siku kama hizi, pamoja na kujishughulisha na ibada za Lailatul Qadri ya kwanza, walikua wamezowea kuhudhuria katika majlisi ya Shekh Haadi Mwenyezi Mungu amrehem katika haram tukufu, kisha wanaenda kwa Shekh (Mula Hamza Zaghir), na wanakwenda kuomboleza kwa Imamu Hussen (a.s) kwa namna waliyo zowea huku wakiwa wamejawa na huzuni”.

Akaongeza kusema kua: “Miongoni mwa aina za uombolezaji zinazo endelea hadi leo, ni kutoka watu wa Karbala wa tabaka zote katika maukibu (msafara) mmoja kuanzia Karbala (hadi Najafu) katika siku aliyo fariki Kiongozi wa Waumini (a.s). Usiku unao fuata pamoja na kuendelea na majaalisi za Husseiniyya, watu wa Karbala walikua wanafanya jambo walilo lirithi kwa watu wa zamani linalo itwa (ham yangu), kulikua na chakula maalumu ambacho watu wa Karbala walikua wanapika na bado wanaendelea kupika hadi leo, nacho ni (wali na maziwa lala), kuna baadhi ya wanahistoria wanaripoti tukio hili kua: Imamu Ali (a.s) alitamani kula chakula hicho siku ya kuuawa kwake, lakini inaonyesha kua Kiongozi wa Waumini alikua anawapenda sana mayatima, alitaka kuwapikia mayatima chakula hicho, na ni sehemu ya wasia wake, kwa hiyo utakuta nyumba zote hupika chakula katika usiku wa ishirini wa Ramadhani na kukigawa kwa mayatima na mafukara, kwa sababu Ali (a.s) alikua baba wa mafakiri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: