Atabatu Abbasiyya yafanya mradi wa (Ruhamaau Bainahum) wa kulea watoto wenye mahitaji ya kibinadamu na wenye mazingira magumu…

Maoni katika picha
Katika hatua muhimu ya kulinda watoto na hatari za mtaani, na kwa ajili ya kuwapa huduma za kifamilia walizo zikosa, Atabatu Abbasiyya tukufu imeanzisha mradi mpya wa kulea watoto wenye mahitaji ya kibinadamu na walio kosa uangalizi wa familia, na wameuita mradi wa (Ruhamaau Bainahum).

Mradi huu ulianzishwa katika mwezi wa Rahma na Maghfira mwezi mtukufu wa Ramadhani, katika muendelezo wa kutoa huduma za kibinadamu.

Mradi huu ulianza kabla ya mwaka mmoja na kundi la vijana wakujitolea, kulea watoto wanao ishi katika mazingira magumu na walio kosa usimamizi wa kifamilia katika mkoa mtukufu wa Karbala.

Vijana hao wamefanikiwa kusaidia wengine na kuwaandaa watoto kuwa watu wema wenye mwelekeo sahihi, na kuwaingiza katika jamii, baada ya kua walikua wamekosa usimamizi wakifamilia na kijamii katika maisha yao, na kuwawezesha kuwa raia wema wanao tii kanuni na sheria za kijamii, pamoja na kuwawezesha kiuchumi na vitu vingine.

Jambo hilo limepelekea Atabatu Abbasiyya iwaingize chini ya hema la Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhakikisha mradi unakua endelevu, na kuchukua idadi kubwa zaidi ya watoto wenye uhitaji wa aina hiyo..

Watoto hao pamoja na wasimamizi wao walikua na kikao maalumu na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ambae amewapongeza na kusisitiza kua Ataba tukufu itawapa kila kinacho hitajika katika kuwalea watoto hao, na aliwapa nasaha, ambapo amewahimiza kujiepusha na ugonvi baina yao na kuheshimu undugu, wanufaike na huduma wanazo pewa na wasome kwa bidii ili waweze kufaulu.

Pia Mheshimiwa Sayyid Swafi aliwashukuru wasimamizi wa mradi na akapongeza juhudi zao, akawataka waongeze juhudi kwa ajili ya kusaidia tabaka hili na kuwarejesha katika mazingira mazuri kwa kutumia njia za kisasa.

Mmoja wa wasimamizi wa mradi huu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mradi wa (Ruhamaau Bainahum) ni mraji unao wahusu watoto, hususan watoto walio ingia katika ajira wakiwa na umri mdogo na wale wanao zurura mitaani, sisi tumeanzisha kituo cha kuwalea na kuwarudishia matumaini waliyo kua wamepoteza kutokana na mazingira waliyo kua wanaishi, na huwa tunawasiliana na familia zao”.

Akaongeza kusema kua: “Hivi sasa mradi una picha mpya, umekua chini ya usimamizi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), ratiba yetu itaendana na njia sahihi za kielimu, na tutawaingiza katika shule za Ameed pamoja na kuwapa semina za kimalezi na kitamaduni zitakazo wajenga katika maisha yao”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeteua kamati maalumu itakayo simamia na kufuatilia mradi huu, na itakayo wajibika na kutekeleza maagizo na maelekezo ya kimalezi na kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: