Ibada za siku hii zimegawanyika katika sehemu tatu:
Sehemu ya kwanza:
- 1- Kuoga, Uoge wakati wa kuzama jua ili uswali Magribaini baada ya kuoga.
- 2- Swala ya rakaa mbili, katika kila rakaa soma Alhamtu na surat Tauhidi mara saba, baada ya kumaliza useme mara sabini: Astaghfirullaha wa atuubu ilaihi. Imekuja katika haditi kua: “Atakaye fanya hivyo hata simama sehemu yake ispokua Mwenyezi Mungu atamsamehe yeye na wazazi wake”.
- 3- Fungua msahafu na uuweke mbele yako kisha umuombe Mwenyezi Mungu kwa kupitia utukufu wa Qur’an hiyo, useme: (Allahumma inni As-aluka bikitaabika-munzal, wa maa fiihi, wa fiihi ismukal-akbaru, wa asmaaukal husna wa maa yukhafu wa yurja an taj’alani min utqaaika mina nnaar) kisha uombe haja zako.
- 4- Weka msahafu mtukufu kichwani kwako na useme: (Allahumma bihaqi hadhal Qur’an, wa bihaqi man arsaltahu bihi, wa bihaqi kullu mu-umin madahtahu fiihi, wa bihaqika alaihim, falaa ahada a’arafa bihaqika minka, bika yaa Allah, mara kumi. kisha useme: Bi Muhammad, mara kumi. Bi Ali, mara kumi. Bi Fatuma, mara kumi. Bil Hassan, mara kumi. Bil Hussein, mara kumi. Bi Ali bun Hussein, mara kumi. Bi Muhammad bun Ali, mara kumi. Bi Jafari bun Muhammad, mara kumi. Bi Mussa bun Jafari, mara kumi. Bi Ali bun Mussa, mara kumi. Bi Muhammad bun Ali, mara kumi. Bi Ali bun Muhammad, mara kumi. Bil Hassan bun Ali, mara kumi. Bil Hujjah, mara kumi.
Kisha uombe haja yako.
- 5- Ziara ya Imamu Hussein (a.s), katika hadithi imekuja kua: “Unapo fika usiku ya Lailatul Qadri, huita mwitaji kutoka katika mbingu ya saba, kutoka katika Arshi na husema: Hakika Mwenyezi Mungu amemsamehe aliye zuru kaburi la Hussein (a.s)” unaweza kusoma ziara hii katika mlango usemao: Ziara ya Imamu Hussein (a.s) katika siku za Lailatul Qadri.
- 6- Kuhuwisha siku hizi tatu kwa kufanya ibada, dhikri na kusoma Qur’an, hadithi inasema: “Atakaye huwisha (fanya ibada) katika usiku wa Lailatul Qadri atasamehewa dhambi zake hata kama zikiwa nyingi kama idadi ya nyota za mbinguni na uzito wa milima na kipimo cha bahari”.
- 7- Kuswali rakaa mia moja, hakika swala hiyo ina fadhila nyingi sana, ni bora asome baada ya Alhamdu surat Tauhidi mara kumi katika kila rakaa.
- 8- Soma dua ifuatayo: (Allahumma innii amsaitu laka abdan daakhiran laa amliku linafsi naf’an walaa dhwarraa, walaa usrifu anha suua…) angalia katika kitabu cha Mafatiihu Janaani.
- 9- Soma dua ya Jausheni kabiir. Angalia katika kitabu cha Mafatiihu Janaani.
Sehemu ya pili: Ibada na dua za siku kumi za mwisho. Usiku wa ishirini na moja ndio usiku wa kwanza wa siku kumi za mwisho, miongoni mwa dua na ibada za siku hizo ni:
- 1- Asome dua hii, ambayo ni dua ya Imamu Swadiq (a.s) katika siku kumi za mwisho: (Allahumma inii audhu bijalaali wajhikal kariim an yanqadhiya anii shahru Ramadhwana au yatlu’al fajru min lailatii hadhihi walaka qibalii dhanbun au tabiatun tuadhibunii alaihi).
- 2- Asome dua ufuatayo, iliyo pokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), aliyo kua akiisoma kila siku katika siku kumi za mwisho: (Allahumma innaka qulta fii kitaabikal munzali, {shahru Ramadhwaana lladhii unzila fiihil Qur’an hudan linaasi wa bayyinaatin minal hudaa walfurqaan}, fa’adhamta hurmata shahri Ramadhwana bimaa anzalta fiihi minal Qur’an, wa khaswastahu bilailatil Qadri, waja’altaha khairan min alfi shahri…) angalia katika kitabu cha Mafatiihu Janaani. Soma mara nyingi dua isemayo: (Yaa mullainal hadiida lidaauda alaihi salaamu, yaa kaashifa dhurri wal karbil idhaam an Ayuubu alaihi salaamu, swali alaa Muhammad wa Aali Muhammad kamaa anta ahluhu, an tuswaliya alaihim ajmaina, waf’al bii maa anta ahluhu, walaa taf’al bii maa anaa ahluhu).
Sehemu ya tatu:
Dua maalumu katika siku hizi:
- 3- Asome dua hii: (Yaa muulija llaili fii nnahaari,wa muulija nnahaari fii llaili, wa mukhrijal hayyi minal mayyit, wa mukhrijal mayyiti minal hayyi…). Angalia katika kitabu cha Mafatiihu Janaani.
- 4- Asome pia dua hii: (Allahumma swali alaa Muhammad wa Aali Muhammad, waqsim lii hilman yasuddu anii baaba jahli wa hudan tamunnu bihi alayya min kulli dhwalaalatin wa ghina tasuddu bihi anii baaba kulli faqrin…). Angalia katika kitabu cha Mafatiihu Janaani.
Ibada za Lailatul Qadri zipo za aina mbili, aina ya kwanza ni ibada za kufanya kila siku, katika siku za Lailatul Qadri, na aina ya pili ni ibada maalumu zinazo fanya kwa muda maalumu ndani ya siku hizo. Sayyid ibun Twausi ameandika katika kitabu cha Iqbaali: kutoka kwa Imamu Baaqir (a.s) anasema: (Atakaye huwisha (fanya ibada) katika usiku wa Lailatul Qadri, atasamehewa dhambi zake hata kama zikiwa nyingi kama idadi ya nyota za mbinguni na nzito kama milima na kipimo cha bahari).
Ibada za jumla katika siku za Lailatul Qadri:
- 1- Kuoga, ni bora uoge wakati wa kuzama jua ili uswali Magharibi na Isha baada ya kuoga kwako.
- 2- Swala ya rakaa mbili, katika kila rakaa soma Alhamdu na surat Tauhidi mara saba, baada ya kumaliza swala useme: (Astaghfiru llaha wa Atuubu ilaihi) mara sabini, utapata thawabu nyingi sana.
- 3- Dua ya kufungua msahafu, katika siku tatu za Lailatul Qadri fungua msahafu na uuweke mbele yako kisha useme: (Allahumma inni As-aluka bikitaabika-munzal, wa maa fiihi, wa fiihi ismukal-akbaru, wa asmaaukal husna wa maa yukhafu wa yurja an taj’alani min utqaaika mina nnaar) kisha uombe haja zako.
- 4- Dua ya kuweka misahafu kichwani na kutawasal kwa Mwenyezi Mungu kupitia misahafu hiyo. Chukua msahafu uufunguwe na kuuweka kichwani kwako na useme: (Allahumma bihaqi hadhal Qur’an, wa bihaqi man arsaltahu bihi, wa bihaqi kullu mu-umin madahtahu fiihi, wa bihaqika alaihim, falaa ahada a’arafa bihaqika minka, bika yaa Allah, mara kumi. kisha useme: Bi Muhammad, mara kuni. Bi Ali, mara kumi. Bi Fatuma, mara kumi. Bil Hassan, mara kumi. Bil Hussein, mara kumi. Bi Ali bun Hussein, mara kumi. Bi Muhammad bun Ali, mara kumi. Bi Jafari bun Muhammad, mara kumi. Bi Mussa bun Jafari, mara kumi. Bi Ali bun Mussa, mara kumi. Bi Muhammad bun Ali, mara kumi. Bi Ali bun Muhammad, mara kumi. Bil Hassan bun Ali, mara kumi. Bil Hujjah, mara kumi. Kisha uombe haja yako, imepokewa katika hadithi kua dua zako zitajibiwa na utakidhiwa haja zako.
- 5- Ziara maalumu ya Imamu Hussein (a.s).
- 6- Kuhuisha usiku wa siku hizo tatu kwa kufanya ibada.
- 7- Kuswali rakaa (100), hakika swala hiyo inafadhila nyingi sana, ni vizuri kusoma Alhamdu na surat Tauhidi (Qul-huwallahu Ahad) mara kumi, katika kila rakaa.