Usiku wa jana, mwezi kumi na tisa Ramadhani ni usiku wenye tukio la kihistoria linalo umiza sana, tukio la kujeruhiwa kwa Kiongozi wa Waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), na mwezi ishirini na moja ndio siku aliyo fariki (a.s), hii ni miongoni mwa kumbukumbu zinazo umiza sana, ni mtihani mkubwa baada ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa kama sehemu ya ratiba yake ya kukumbuka siku za huzuni, imefanya majlisi ya kuomboleza ambayo hufanywa kila mwaka kwa ajili ya kukumbuka msiba huu unao waumiza Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao, ulio tokea siku kama hizi mwaka wa 40 hijiriyya.
Majlisi ya kuomboleza inafanywa kila siku katika siku ndani ya siku tatu hizi tukufu, katika ukumbi wa utawala, hujumuisha utoaji wa muhadhara wa kidini ukitanguliwa na kisomo cha Qur’an tukufu, mada zinazo tolewa zinahusu tukio la kuumiza kwa waislamu baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w), ambalo ni tukio la kujeruhiwa na kufariki kwa Imamul-Mutaqiina na Ya’asuubu Dini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), tukio lililopangwa na muovu wa waovu Abdurahmaan bun Muljim (laana iwe juu yake) katika mji wa Maka akiwa na kundi wa watu wake Makhawaarij na akaenda kufanya (unyama huo) katika msikiti mtukufu wa Kufa, pia huongelewa mambo mbalimbali kuhusu maisha ya Imamu Ali (a.s), mtu wa pili kwa utukufu baada ya Mtume (s.a.w.w).