Kufuatia kumbukumbu ya kifo cha baba wa mayatima: Atabatu Abbasiyya tukufu yaandaa futari ya pamoja kwa familia na mayatima wa mashahidi wa Hashdi Sha’abi…

Maoni katika picha
Ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi wa Ramadhani ina orodha ndefu, katika orodha hiyo kuna kipengele cha program za mayatima na familiazao, hususan walio jitolea nafsi zao na kuitikia wito wa taifa na Marjaiyya tukufu, wakajitolea damu zao kwa ajili ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu, mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) unaandaa futari ya pamoja ya mayatima na familia zao, wanao ishi majumbani au katika taasisi za kulea mayatima, program hii imepangwa kwa kushirikiana na watu wanao saidia na kufadhili jamii hii.

Uandaaji wa futari hii unafanyika sambamba na kumbukumbu ya kifo cha baba wa mayatima Imamu Ali (a.s), ni moja ya jambo ambalo hupewa umuhimu mkubwa na kitengo cha mgahawa (mudhifu) ndani ya mwezi wa Ramadhani, mwezi wa mapenzi, kutoa, na kutembeleana, mwezi wa kuwasidia mayatima na wajane –hususan mayatima wa Hashdi Sha’abi na jeshi la serikali- ili na wao wahisi furaha na utulivu wa nafsi, jambo hili limesisitizwa sana na dini ya kiislamu, imehimiza kuwalea na kuwajali.

Mayatima na familia zao wameonyesha furaha nawameishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwafanyia jambo hili katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kumbuka kua program hii ni muendelezo wa program zingine kama hizi zilizo fanywa na Atabatu Abbasiyya katika mwezi huu mtukufu, kwa ajili ya kuwafanyia ukarimu kutokana na kujitolea kwao, hakika Ataba tukufu imeandaa ratiba maalumu ya mwezi wa Ramadhani yenye vipengele vingi, kikiwemo kipengele hiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: