Tangazo la hivi punde: Ziara ya bure na usafiri ni wa basi za kisasa zenye viyoyozi kwa ajili ya kuhuisha Lailatul Qadri ya mwisho katika malalo ya Askariyyaini (a.s).

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unawatangazia watu wote wanaopenda kwenda kufanya ibada za Lailatul Qadri ya mwisho katika haram ya Maimamu wawili wa Askariyyaini (a.s) katika mji mtukufu wa Samaraa wafike kesho Alkhamisi (22 Ramadhani 1439h) sawa na (7 Juni 2018m) saa saba Adhuhuri mbele ya jengo la Imamu Hassan Askariy (lililo kua likijulikana zamani kama hoteli ya Dalla), lililopo katika eneo la mlango wa Bagdadi (Baabu Bagdadi), kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda katika mji mtukufu wa Samaraa, kuwazuru maimamu wawili wa Askariyyaini (a.s) na kufanya ibada za Lailatul Qadri tukufu, muda wa kurudi ni baada ya swala ya Alfajiri.

Tambua kua usafiri ni bure kwa mazuwaru wote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: