Kituo kimebainisha kua; ni wajibu wetu kupongeza kazi kubwa inayo fanywa na Ataba tukufu pamoja na taasisi za Qur’an katika nchi yetu kipenzi, miongoni mwa juhudi zao za wazi za kuwaandaa watu walio fanya vizuri katika mradi ndani ya mwaka huu, kama tulivyo ona mwaka huu mikoa tofauti imekua na ushiriki mzuri (katika mashindano ya Qur’an) tofauti na miaka ya zamani, hapa tunatanguliza shukrani zetu kwa watumishi wote.
Kituo kikasema kua kuna mambo mengi tunapenda kuyafafanua, nayo ni:
- 1- Kamati imefuta maombi ya watu wote walio tuma video zao mara mbili, ispokua wale walio piga simu na kuelezea sababu ya kufanya hivyo kua ni kutokana na kasoro zilizo kuwepo za sauti au picha.
- 2- Kamati imefuta maombi ya watu wote walio tuma audio peke yake.
- 3- Kamati imefuta maombi ya watu wote walio zaliwa kabla ya mwaka (2000).
- 4- Majina yaliyo tangazwa ni yale ya walio shinda katika mtihani wa kwanza, na watashiriki mtihani wa pili katika mji mtukufu wa Karbala kabla ya kuanza mradi mwishoni mwa mwezi huu wa sita.
- 5- Walio kubaliwa wanaweza kutuma meseji katika namba hii (07740314710) kwenye telegram. Na wataona majina ya walio kubaliwa.