Ibada za Lailatul qadri ya tatu na fadhila zake…

Maoni katika picha
Riwaya zimetofautiana katika kuainisha usiku wa Lailatul Qadri, kati ya usiku wa kumi na tisa, ishirini na moja na ishirini na tatu wa mwezi wa Ramadhani, hadithi nyingi zinaonyesha kua usiku wa ishirini na tatu ndio usiku wa Lailatul Qadri, kuna ibada muhimu zimesuniwa kufanywa katika siku hizo tatu zilizo tajwa.

Usiku wa ishirini na tatu una fadhila kubwa zaidi ya siku zingine, kufanya ibada katika usiku huo ni sawa na kufanya ibada katika miezi elfu moja, kuna riwaya nyingi zinazo sisitiza kufanya ibada zaidi katika usiku huo, pamoja na kuashiria kua Lailatul Qadri ni moja, ambayo kuna iktilafu katika kuibaini, lakini siku hizi tatu (19-21-23) huitwa siku za Lailatul Qadri, hivyo itakua ni moja kati ya siku hizo.

Katika usiku huo hushuka Malaika kwa Walii wa Mwenyezi Mungu Imamu Mahdi (a.f) na kumuonyesha mambo waliyo pangiwa waja, naye hutoa ayatakayo na hubakisha ayatakayo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, ni vizuri kutawasal kwa kupitia kwa Imamu (a.s) na kumuomba awe muombezi wako kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kubadilisha Qadhaa, na kukufanyia hali ya duniani na akhera kua nzuri zaidi.

Ibada za usiku huu zimegawanyika sehemu tatu:

Sehemu wa kwanza: Ibada ambazo zinapatikana katika siku zingine.

Sehemu ya pili: Ibada ambazo zinapatikana katika siku kumi za mwisho, tumesha zielezea, unaweza kuangalia katika mtandao: https://alkafeel.net/news/index?id=6864

Sehemu ya tatu: Ibada na dua maalumu za usiku huu:

Na ibada za usiku huu zimegawanyika sehemu tatu:

Sehemu wa kwanza: Ibada ambazo zinapatikana katika siku zingine.

Sehemu ya pili: Ibada ambazo zinapatikana katika siku kumi za mwisho, tumesha zielezea, unaweza kuangalia katika mtandao: https://alkafeel.net/news/index?id=6864

Sehemu ya tatu: Ibada na dua maalimu za usiku huu.

Dua maalumu za usiku huu ni:

  • 1- Kusoma surat Ankabuut na surat Ruum.
  • 2- Kusoma surat Dukhaan.
  • 3- Kusoma surat Qadri mara elfu moja.
  • 4- Katika usiku huu usome dua hii: (Yaa Rabi Lailatul Qadri wa jaailuha khairan min alfi shaharin, wa Rabi llaili wa nnahaar, waljibaali walbihaari, wa dhulami wal-anwaari, wal-ardhi wa samaai, yaa baariu yaa muswawwiru, yaa hannaanu yaa mannaanu, yya Allahu yaa Rahmaanu, yaa Allahu yaa Qayyuumu, yaa Allahu ya Badii’u, yaa Allahu yaa Allahu yaa Allahau, lakal-asmaaul husnaa, wal-amthaalul ulya, wal-kibriyaau wal aalaau, as-aluka an-tuswalliya alaa Muhammad wa Aali Muhammad, wa-an taj-ala ismii fii hadhihi llailati fii suadaa, wa ruuhii ma’a shuhadaa, wa ihsaanii fii iliyyiin, wa isaa-atii maghfuurah, wa an-tahaba lii yaqiinan tubaashiru bihi qalbii, wa iimaanan yudh-hibu shakkaka annii, wa tardhiyanii bimaa qasamta lii, wa aatinaa fii dun-ya hasanatan wa fil-aakhirati hasanatan, wa qina adhaabal hariiqi, warzuqnii fiiha dhikraka wa shukraka wa raghbata ilaika, wal-inaabata wa taubata wa taufiiqa limaa wafaqta lahu Muhammadan wa Aala Muhammadin alaihi salaam).
  • 5- Na usome dua hii pia: (Allahumma mdudlii fii umrii, wa ausi’ilii fii rizqii, wa aswiha jismii, wa ballighnii amalii, wa inkuntu minal-ashqiyaai famhunii minal ashqiyaai, waktubnii mina suadaai, fainnaka qulta fii kitaabikal munzali, alaa Nabiyyikal mursali swalawaatuka alaihi wa aalihi: [Yamhu Llahu maa yashaau wa yuthbitu wa indahu ummul-kitaabu]).
  • 6- Usome dua hii ya Imamu Mussa bun Jafari Alkaadhim (a.s): (Allahumma ij’al fiimaa taqdhi wa fiimaa tuqaddiru minal amril mahtuumi, wa fiimaa tafruqu minal amril hakiim fii lailatil qadri, minal qadhaai ladhii laa yuraddu walaa yubaddalu, an-taktubanii minal hujjaaji baitikal haraam fii aami hadha, almabruuri hajjuhum, almashkuuri sa’ayuhum, almaghfuuri dhunuubuhum, almukaffari anhum sayyiaatihim, waj-al fiimaa taqdhii wafiimaa tuqaddiru an-tutwiila umrii, wa tuwasialii fii rizqii).
  • 7- Na usome dua hii iliyopo katika kitabu cha Iqbaali: (Yaa baatwinan fii dhuhuurihi, wa yaa dhwaahiran fii butuunihi, yaa baatwinan laisa yakhfaa, wa yaa dwaahiran laisa yuraa, yaa mausuufan laa yablughu bikainuunatihi mausuufun, walaa hadun mahduudun, yaa ghiyaaban ghaira mafquudin, wa yaa shaahidan ghaira mash-huudin, yutlabu fayuswaabu, walam yakhlu minhu samaawaatu wal-ardhu wa maa bainahumaa twarafata ainin, laa yudraku bikaifin, walaa yu-ayyanu bi-ainin walaa bihaithin, anta nuuru nnuuri, wa Rabbul Arbaabi, ahatta bijami’il umuuri, subhaana man laisa kamithlihi shaiun wa huwa samiiul baswiiru, subhaana man huwa haakadha walaa haakadha ghairuhu). Kisha omba haja yako.
  • 8- Soma dua ya Maqaarimul Akhlaaqi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: