Mwezi wa Ramadhani katika kumbukumbu ya Karbala: Lailatul Qadri na uhuishwaji wake…

Maoni katika picha
Kwa sababu Karbala ni mlango miongoni mwa milango ya Mwenyezi Mungu katika Ardhi yake, usipo kua ndio mkubwa na ulio karibu yake zaidi basi inautukufu wa pekee, kwani uwanja wa toba na istighfaar umekuwepo tangu vita ya Twafu, nuru ya Mwenyezi Mungu imeendelea kuangaza katika ardhi ya Karbala kwa kuwepo kubba la bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s).

Baada ya uliyo soma, Je! Unaweza kufikiria inakuaje siku iliyo teremswa Qur’an tukufu katika mji unao angaziwa na nuru ya Mwenyezi Mungu kwa mamia ya miaka?! Je! Unaweza kufikiria Lailatul Qadri ukovipi katika nyoyo za watu wa Karbala?!.

Mmoja wa watu wa Karbala anaelezea usiku huu (wa Lailatul Qadri) ulivyo kua ukienziwa katika miaka ya sitini na sabini, naye ni Ustadh Ali Khabbaaz kiongozi wa idara ya habari ya Atabatu Abbasiyya tukufu: “Miongoni mwa mambo makubwa kwa watu wa Karbala ndani ya Ramadhani ni kuhuisha Lailatul Qadri, ndani ya uwanja wa haram tukufu (nakusudia uwanja wa haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi –a.s-) vikifanywa vikao vya ibada ya Lailatul Qadri na kuinua taa, watu wote wa Karbala walikua wanahudhuria, hivyo tunacho kiona leo, watu kuja kwa wingi kusoma dua na kufanya majaalisi Husseiniyya na baadhi ya vitu vingine, ni muondelezo wa urithi huu wa kuhuisha usiku huu mtukufu kwa mamia ya miaka, uhuishaji wa masiku haya haufanyiki katika haram mbili peke yake, bali unafanyika misikitini katika Husseiniyya na kila sehemu”.

Akaongeza kusema kua: “Kuna utamaduni ulio zoweleka kwa watu wa Karbala katika siku kama hizi la Lailatul Qadri hasa tarehe 23 Ramadhani, utakuta wanashindana kufuturisha, jambo hili hufanyika tangu mwanzo wa mwezi, lakini katika siku hiyo hutiliwa umuhimu zaidi, watu wote, mafakiri na matajiri huandaa futari na kuigawa, jambo hilo huitwa Qadri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: