Wanarukuu, kusujudu na kusoma dua hadi inachomoza Alfajiri… Ibada za Lailatul Qadri ya tatu (katika picha).

Maoni katika picha
Katika usiku mtukufu ulio jaa mazingira mazuri ya kiroho na kiibada, makundi ya waumini wamefanya ibada za usiku wa tatu wa Lailatul Qadri ambao Qur’an imeutaja kua ni bora zaidi ya miezi elfu moja, waumini wamekusanyika kuhuisha usiku huu mtukufu katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ambao kuwazuru ni moja ya ibada muhimu ndani ya usiku huu, waumini hufunga safari ya kuja katika mji wa Karbala katika usiku huu na katika siku mbili zilizo pita, kutokana na umuhimu wa Lailatul Qadri kiroho na kiimani, kila mu-umin hutaka azipate fadhila za usiku huo.

Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na uwanja wa katikati ya haramu mbili zimefurika waumini walio kuja kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Karbala kwa ajili ya kuhuisha usiku huu mtukufu, ambapo huanza kwa kusoma dua Iftitaahi na dua Jausheni Alkabiir pamoja na dua ya kuinua misahafu, sambamba na kusoma baadhi za sura za Qur’an tukufu na kuswali pamoja na ibada zingine nyingi ambazo ni maalumu katika usiku huu, ibada hizo wanafanywa kwa vikundi kama ilivyo katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu au mmoja mmoja, wakiwa na matarajio makubwa kwa Mwenyezi Mungu mtukufu akubali ibada zao na ailinde Iraq na raia wake pamoja na maeneo matukufu.

Watumishi wa Ataba mbili tukufu wamefanya juhudi kubwa ya kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru na kuwawezesha kufanya ibada kwa amani na utulivu.

Kumbuku kua usiku wa ishirini na tatu ni miongoni mwa siku tukufu zaidi katika siku za Lailatul Qadri, kufanya ibada katika usiku huo ni sawa na kufanya ibada katika miezi elfu moja, zimepokewa riwaya nyingi zinazo sisitiza umuhimu wa kufanya ibada katika usiku huu, bila kusahau usiku wa Lailatul Qadri ni mmoja na kuna tofauti ya kuuainisha, lakini siku hizi tatu (19-21-23) huitwa siku za Lailatul Qadri, hivyo itakua ni miongoni mwa siku hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: