Vikao vya usomaji wa Qur’an vyafanywa na idara ya maelekezo ya dini ya wanawake kila siku ndani ya mwezi mtukufu…

Maoni katika picha
Usomaji wa Qur’an unafadhila kubwa kila siku ndani ya mwaka na katika mwezi wa Ramadhani faida na thawabu zake ni kubwa mno, kusoma aya moja ndani ya mwezi wa Ramadhani unaandikiwa thawabu za kusoma Qur’an nzima katika miezi mingine.

Kutokana na utukufu huo na kufuatia ratiba iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, idara ya maelekezo ya dini iliyo chini ya kitengo cha habari na utamaduni, imefanya mahafali na vikao vya usomaji wa Qur’an pamoja na mashindano ya Qur’an ndani na nje ya Ataba tukufu, wametumia uwezo wote katika kufanikisha ratiba hiyo na chini ya wasomi wakubwa wa Qur’an wenye uzowefu mkubwa katika maswala ya Qur’an.

Kumekua na vikao vitatu vya usomaji wa Qur’an upande wa wakina dada, vinavyo fanywa katika sardabu ya Imamu Hussein (a.s), vya wakina dada wa Zainabiyyaati wanao fanya kazi katika Ataba tukufu pamoja na mazuwaru, asubuhi kuna vikao viwili na kingine Adhuhuri (mchana), hushiriki wasomaji kutoka katika idara tuliyo taja na wengine kutoka katika Madrasat Fadak Zaharaa (a.s) ya Qur’an, pia idara hii hufanya vikao vya usomaji wa Qur’an kwa upande wa wakina dada katika Maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f), na husimamiwa na wakina dada wa Madrasat Fadak Zaharaa (a.s), pia kuna kikao cha usomaji wa Qur’an kwa wanawake katika majengo ya Abbasi (a.s) ya makazi, chini ya usimamizi wa mmoja wa watumishi wa idara, zaidi ya hapo kuna vikao vya usomaji wa Qur’an vinavyo fanywa na baadhi ya watumishi katika nyumba zao.

Vikao hivyo vya usomaji wa Qur’an tukufu, haviishii kusoma tartiil peke yake, bali kuna mambo mengi yanayo fungamana na visomo hivyo, kama vile:

  • 1- Kusahihisha usomaji wa washiriki kwa kuwapa nafasi kubwa ya kusoma.
  • 2- Kubainisha baadhi ya hukumu za usomaji na tajwidi ili kurekebisha usomaji wao.
  • 3- Kutafsiri baadhi za aya zinazo ashiria kubainisha sheria au maelekezo ya ki-akhlaqi, au kuimarisha uhusiano na Mwenyezi Mungu ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani pamoja na miezi mingine, na uhusiano huo huonekane katika mwenendo wa maisha, sawa iwe katika nyanja ya ibada kwa kufanya idaba za faradhi na kuzipupia, au katika nyanja ya maisha, kama vile namna ya kuamiliana na mtu, familia au jamii, au namna unavyo ishi na marafiki zako unao fanya nao kazi, au namna unavyo himiza wengine kuheshimu sheria na kanuni ambazo wewe unaziheshimu na kuzitekeleza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: