Miongoni mwa kumbukumbu za mwezi wa Ramadhani: Tarehe ishirini na nne ya mwezi wa Ramadhani alishuka Malaika Jibrilu (a.s) na amri ya kuozeshwa kiongozi wa waumini bibi Zaharaa (a.s)…

Maoni katika picha
Terehe ishirini na nne ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka wa pili hijiriyya, alikuja Malaika Jibrilu (a.s) na jambo la kuozeshwa bibi Fatuma (a.s), ili Mtume amuozeshe kwa Ali bun Abu Twalib (a.s).

Jibrilu (a.s) alikua na nafasi kubwa katika kuolewa kwa bibi Fatuma (a.s), alionekana mara nyingi katika swala hili, kutokana na umuhimu wake wa kujalia uimamu kua katika familia hii na kuwafanya waendane na uteule wa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu.

Mwenyezi Mungu anasema: (Hakika Mwenyezi Mungu alimteua Adam na Nuhu na ukoo wa Ibrahim na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote. * Ni wazao wao kwa wao; na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia na mwenye kujua).

Hakika kuonekana mara kwa mara kwa Jibrilu (a.s) katika swala hili, ni kwa kuwa wao ni wateule wa kuendeleza nuru ya utume na njia ya sheria na kuunda dola ya haki na uadilifu, na kuufanya uislamu kua juu ya dini zote katika zama za Mahdi (a.f) atokanaye na kizazi cha Fatuma (a.s).

Kutoka kwa Ummu Salama, na Salmani Muhammadiy, na Ali bun Abu Twalib (a.s) wote wamepokea kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), ya kwamba alisema: (Alinijia Jibrilu, akasema: Amani iwe juu yako na rehma za Mwenyezi Mungu ewe Nabii wa Allah, kisha akaweka mikononi kwangu kitambaa cheupe cha hariri kutoka peponi, kikiwa kimeandikwa mistari miwili kwa nuru. Nikasema: ewe rafiki yangi Jibrilu, hii hariri ni yanini, na maandishi haya ni ya nini? Jibrilu akasema: Ewe Muhammad hakika Mwenyezi Mungu aliwaangalia waja wake wa ardhini akakuchagua wewe kua Mtume wake, kisha akaangalia ardhini kwa mara ya pili, akakuchagulia ndugu na waziri na rafiki yako, umuozeshe mwanao Fatuma. Nikasema: Rafiki yangu ewe Jibrilu ni nani huyu mtu? Akasema: Ewe Muhammad ndugu yako wa duniani na akhera ni mtoto wa Ammi yako katika nasaba Ali bun Abu Twalib).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: