Maahadi ya Qur’an tukufu yafungua mlango wa usajili kwa ajili ya mradi wa masomo ya Qur’an katika kipindi cha kiangazi…

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuanza kwa usajili wa masomo ya Qur’an ya kiangazi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari (upili), usajili utaendelea hadi tarehe kumi na tano ya mwezi huu wa sita, masomo yatakayo fundishwa ni Qur’an tahfiidh, Fiqhi, Akhlaqi na Aqida, masomo yataanza baada ya sikukuu ya Idil-Fitri tukufu.

Usajili unafanyika kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika ofisi za Maahadi zilizopo katika mkoa wa Karbala karibu na haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mkabala na mlango wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s), pamoja na kwenye matawi yake yaliyopo mikoani, usajili unafanyika kwa kujaza fomu ya maombi na kutoa picha ya muombaji pamoja na kopi ya kitambulisho.

Kumbuka kua masomo haya yamepangwa kwa ajili ya kujenga utamaduni wa kushikamana na Qur’an na kuiingiza katika nafsi za vijana pamoja na kutengeneza kizazi kinacho jua Qur’an, kama sehemu ya kufanyia kazi maneno ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) yasemayo: (Wafundisheni watoto wenu mambo matatu: kumpenda Mtume wenu na kuwapenda watu wa nyumba yake na kusoma Qur’an), semina hizi hufanywa kila mwaka, baada ya kumaliza msimu wa masomo na wamesoma na kuhitimu katika semina hizi maelfu ya wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: