Atabatu Abbasiyya tukufu yagawa vikapu vya chakula vya mwezi wa Ramadhani kwa familia za mashahidi wa hashi Sha’abi…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba za kusaidia familia za mashahidi wa Iraq walio jitolea nafsi zao kwa ajili ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu, na kuwakirimu pamoja na kuenzi damu zao takatifu ndani ya mwezi huu mtukufu mwezi wa Ramadhani, Atabatu Abbasiyya kupitia kitengo cha dini kama kawaida yake katika mwezi huu, imetoa vikapu vya chakula vya mwezi wa Ramadhani kwa familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi na mamilia za wasio jiweza katika mkoa mtukufu wa Karbala.

Vikapu hivyo vya chakula vimesheheni aina tofauti za vyakula vinavyo hitajiwa na mtu aliye funga katika mwezi huu mtukufu, kazi hii ya kugawa chakula ni sehemu ya ratiba kubwa ya kuwatembelea majeruhi na familia za mashahidi katika miji yote ya Iraq, kwa ajili ya kudumisha mawasiliano nao na kusaidia mahitaji yao, na kuwaonyesha kua tunawajali sambamba na kuwapa zawadi kutokana na kujitolea kwa watoto wao, ratiba hii ilipangwa kwa ajili ya kuitikia wito wa Marjaa dini mkuu aliye taka kuzisaidia familia hizi ili kuwapunguzia uchungu wa maisha.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalumu ya kuwapa zawadi familia za mashahidi toka ilipo tolewa fatwa tukufu ya jihadi ya kujilinda hadi leo, wamesha saidia na kutoa usimamizi kwa maelfu ya familia chini ya maelekezo ya Marjaa dini mkuu kwa ajili ya kudumisha ushindi dhidi ya makundi maovu ya kigaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: