Umuhimu wa kuwekwa saa hizi unatokana na ukweli kua mazuwaru na watumishi wanahitaji kufahamu muda kila dakika, saa zilizo kuwepo mwanzo zilikua hazitoshi, pia saa hizi zinasaidia kuboresha utendaji katika ukumbi wa haram tukufu, saa zimewekwa kulingana na aina ya kila saa, zile saa za upande mmoja na za pande mbili, zimepangwa katika ukumbi mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika milango ya Ataba pamoja na katika Sardabu zinazo fungamana na ukumbi wa haram, zimewekwa pia na katika ukumbi wa Imamu Hassan na katika mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya tukufu na katika majengo ya nje zikiwemo sehemu za kuweka viatu na vifaa mbalimbali (amanaati).
Saa hizi zinasifa za pekee, miongoni mwa sifa zake ni:
- 1- Zimetengenezwa na kampuni ya (Perrot) ya kijerumani, kampuni inayo sifika kwa kutengeneza saa nzuri, nayo ndio walio tengeneza saa kubwa iliyopo katika Atabatu Abbasiyya na ile iliyopo katika Atabatu Husseiniyya tukufu, pia ndio walio tengeneza saa kubwa iliyopo katika haram tukufu ya Maka.
- 2- Vifaa vya kubainisha muda wa eneo husika vimetengenezwa Uswisi pamoja na vifaa vingine vya ndani ya saa, vimetengezezwa na kampuni ya (MobaTime) ya Uswisi pamoja na mzunguko wa saa umepangiliwa na kambuni hiyo.
- 3- Zinamuonekano mzuri na zinafanana na saa zilizopo katika Atabatu Abbasiyya tukufu lakini hizi zina umbo dogo.
- 4- Saa zote muda wake umepangwa sawa sawa na saa kubwa ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- 5- Namba zake ziko wazi na unaweza kuzisoma kwa mbali.
- 6- Kila saa inamwanga wa ndani unao muwezesha mtu kuisoma hata akiwa mbali.
- 7- Kila saa imeonganishwa na sistim ya muda ya kimataifa kupitia setlait.
Kiongozi wa idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Farasi Hamza ameelezea kuhusu ufungaji wa saa hizi kua: “Saa zote zimeunganishwa katika mfumo maalumu ulio tengenezwa na idara ya mawasiliano (IP Network) wa kompyuta, chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, na zimeunganishwa na sistim ya (Time Server) ya eneo hili kama msingi mkuu wa (GPS) ya setlait inayo fanya kazi kwa mujibu wa Jografia ya dunia na kuainisha muda kimataifa, pia zinaweza kuunganishwa na mtandao wa Intaneti wa kimataifa kama msingi wa pili wa kuainisha muda”.
Akaongeza kusema kua: “Mtandao wa kompyuta pamoja na saa zilizo onganishwa nao unaweza kuendeshwa kwa kutumia (Clocks Management Server) kama njia ya ziada ya kuseti saa hizi, kuzisimamia na kupangilia mwanga wake wa ndani na sistim ya (Data Center) ipo katika kituo cha mawasiliano”.