Mihadhara ya dini inayo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa watumishi wake ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani…

Maoni katika picha
Ni desturi ya kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya mwezi wa Ramadhani kutoa mihadhara ya kidini kwa watumishi wa malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mihadhara hiyo hufanywa kila siku kwa muda wa saa moja ndani ya Sardabu (ukumbi wa chini) wa Ataba tukufu, hutolewa mada tofauti zinazo lenga kunufaika na mwezi huu mtukufu.

Shekh Swalahu Karbalai ambaye ni rais wa kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu amefafanua kua: “Utoaji wa mihadhara hii ni sehemu ya ratiba tuliyo panga kwa ajili ya kuhuisha siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi huu wa pekee ambao ni bora kushinda miezi yote na siku zake ni bora kuliko siku zote, pumzi katika mwezi huu unaandikiwa thawabu za kufanya tasbihi, na ukilala unaandikiwa thawabu sawa na anaye fanya ibada, unafadhila nyingi na neema kubwa, zilizo tajwa katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na hadithi za mtume (s.a.w.w), mwezi ambao iliteremswa Qur’an katika usiku wa Lailatul Qadri, ambao ni usiku bora kushinda miezi elfu moja… na mengineyo mengi matukufu katika mwezi huu, hivyo ni jambo jema kwetu kutoa mafundisho ya dini kwa watumishi wa haram hii tukufu ndani ya mwezi huu, kwa kuwafafanulia baadhi ya mambo wanayo kutana nayo wawapo kazini au nje ya kazi, na kuelezea baadhi ya matukio ya kihistoria ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) pamoja na kuzielezea siku tukufu”.

Akaongeza kusema kua: “Hali kadhalika hua kuna wakati wa kujibu maswali kutoka kwa watumishi yanayo husu mwezi wa Ramadhani au jambo lingine lolote, na majibu hutolewa kwa wazi ili watu wote wapate faida”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu kila mwaka huandaa ratiba maalumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani yenye vipengele mbalimbali, ikiwemo mihadhara ya kifiqhi, kwa ajili ya kufafanua mambo yanayo husiana na hukumu za funga na mengineyo, na kujibu maswali kutoka kwa watumishi na mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: