Uongozi wa jengo la kibiashara la Afaaf upande wa wanawake wapanga siku maalumu ya kugawa nguo kwa mayatima na familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi…

Maoni katika picha
Miongoni mwa vipengele vya ratiba ya mwezi wa Ramadhani, Atabatu Abbasiyya tukufu imepanga siku maalumu ya kugawa nguo kwa familia na mayatima wa Hashdi Sha’abi, walio jitolea nafsi zao na wakaitikia wito wa taifa na Marjaiyya na kumwaga damu zao kwa ajili ya kubakiza heshima ya Iraq na maeneo matukufu.

Uongozi wa jengo la kibiashara la Afaaf chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wameandaa makundi ya mayatima na familia zao, kutoka katika nyumba binafsi au katika vituo na taasisi za kulea mayatima, chini ya utaratibu maalumu ulio wekwa kwa kushirikiana na kamati inayo simamia swala hili, pamoja na taasisi za kiraia zinazo fanya shughuli za kijamii kitaifa.

Bibi Ummu Hussein kiongozi wa jengo la kibiashara la Afaal upande wa wanawake amesema kua: “Hakika jambo hili lilianza tangu kutolewa kwa fatwa tukufu ya Marjaiyya, aliyo toa karibu na siku za Idil-Fitri tukufu, iliyo himiza kuonyesha mapenzi na huruma pamoja na kujenga uhusiano mzuri na mayatima pamoja na wajane –hususan mayatima wa mashahidi wa Hashdi Sha’abi na wanajeshi wa serikali- ili nao wapate amani katika nafsi zao, na kuingiza furaha katika nyoyo za watu walio jitolea kulinda mafundisho ya dini yetu ya kiislamu”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika mradi huu unalenga kupunguza uchungu wa matatizo ya kiuchumi na kijamii kwa familia zenye mahitaji, pamoja na kuboresha maisha ya familia hizo”.

Kumbuka kua jambo hili ni miongoni mwa harakati nyingi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa familia hizi katika mwezi huu mtukufu, hii inaonyesha namna inavyo jali kujitolea kwao, hakika Ataba tukufu iliandaa ratiba maalum ya mwezi wa Ramadhani yenye vipengele vingi kikiwemo kipengele hiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: