Idara ya khutuba za wanawake inaendelea na ratiba yake ya mwezi wa Ramadhani na yasisitiza kua wamepata mafanikio mazuri…

Maoni katika picha
Idara ya khutuba za wanawake ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kua ratiba yake ya mwezi wa Ramadhani inayo endelea kila siku ndani ya wezi huu mtukufu imekua na mafanikio makubwa, imepata mwitikio mzuri na ushiriki mkubwa wa mazuwaru, pamoja na idadi kubwa ya ushiriki inayo endana na utukufu wa mwezi huu tulio itwa katika ugeni wa Mwenyezi Mungu mtukufu. Makamo kiongozi mkuu wa idara hiyo (Ummu Hassan) akasema kua: “Hakika ratiba yetu ya mwezi wa Ramadhani ya mwaka huu, ni nzuri kwa kila mshiriki, imepangwa kutokana na siku za mwezi mtukufu pamoja na kuweka vipengele maalumu katika baadhi za siku zenye matukio maalumu, kama vile siku ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s), siku ya kifo cha bibi Khadijatu Kubra na kifo cha Imamu Ali (a.s).

Akabainisha kua: “Sifa kubwa ya ratiba yetu ni vikao vya usomaji wa Qur’an, ambavyo vinafanywa kila siku asubuhi katika Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s), ambayo ni miongoni mwa sehemu zilizo ongezwa katika upanuzi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), vikao hivi vinalenga kuwafungamanisha watu na Qur’an tukufu pamoja na kutengeneza kizazi chenye uwelewa mzuri wa Qur’an na kinacho heshimu siku za Lailatul Qadri”.

Akaongeza kua: “Vikao hivi vinahusisha kisomo cha Qur’an kuanzia saa nne hadi saa sita asubuhi, husomwa juzuu moja la Qur’an tukufu na kufafanua maana za baadhi ya maneno ya aya za Qur’an zilizo somwa, sambamba na kutoa nafasi ya maswali na majibu, na kufafanua baadhi za hadithi za kiitikadi zinazo himiza tabia njema za kiislamu kutoka kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), zinazo fungamana na aya tukufu za Qur’an zilizo somwa katika juzuu husika, pamoja na kufafanua baadhi ya matukio ya kihistoria yaliyo tokea ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na baadhi ya visa vilivyo tajwa ndani ya Qur’an tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: