Miongoni mwa harakati za Qur’an ndani ya mwezi wa Ramadhani: Maahadi ya Qur’an tukufu yaratibu usomaji wa Qur’an tartiil na hifdhu…

Maoni katika picha
Kutokana na kauli ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Wa adabisheni watoto wenu mambo matatu: Kumpenda mtume wenu, na kuwapenda watu wa nyumbani kwake, na kusoma Qur’an, hakika waijuao Qur’an watakua katika kivuli cha Mwenyezi Mungu siku ambayo hakuna kivuli ispokua hicho), idara ya kuhifadhi Qur’an katika Maahadi ya Qur’an chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeendesha usomaji wa Qur’an tartiil na hifdhu kwa watoto na vijana, nayo ni miongoni mwa orodha ya visomo inavyo visimamia katika mkoa wa Karbala na nje ya mkoa huu.

Visomo hivyo vinafanyika katika majengo ya makazi ya Abbasi (a.s), na kushiriki idadi kubwa ya watoto na vijana, kwa lengo la kukomaza hifdhu zao na kuwapa fursa ya kuonyesha uwezo wao katika kuhifadhi, na kuifanya nguvu ya ujana itumike katika kukipenda kitabu cha Mwenyezi Mungu na kujifundisha maisha kutokana na mafundisho ya aya zake na kuchota maarifa katika mto wake usio kauka, Mwenyezi Mungu ameotesha dini katika nyoyo zao toka wakiwa wadogo na akaizungushia ngome ya utakasifu na imani, hauja wahi kupata hasara umma ulio shikamana na aya za Mwenyezi Mungu na kuzifanya kua muongozo wao, umma huo ulifanikiwa duniani kabla ya akhera, na umepata hasara umma ulio jitenga na Qur’an.

Visomo hivyo vilipata muitikio mkubwa wa watoto na vijana, wakiwa na imani ya kufungua uwezo wao wa kiakili, na kukuza uwelewa wao pamoja na kuonyesha uwezo wao na maendeleo yao kimasomo.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya iliandaa ratiba maalumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, iliyo jumuisha kipengele cha usomaji wa Qur’an na mashindano ya Qur’an na vinginevyo, sawa iwe katika Maahadi au katika matawi yake yaliyopo katika mikoa mingi ya Iraq, hii ni kwa ajili ya kueneza utamaduni wa kusoma Qur’an tukufu, na kusaidia kuisoma Qur’an yote katika mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: