Ofisi ya Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani imetangaza kiwango cha pesa inayo faa kulipwa kwa ajili ya Zakatul-Fitri mwaka huu, ambacho ni (1,500) elfu moja na mia tano dinari za Iraq kwa mtu mmoja kwa ajili ya funga ya mwezi wa Ramadhani ya mwaka huu (1439h).
Kiwango cha Zakatul-Fitri ni pishi moja kwa mtu, pishi moja ni sawa na kilo tatu za ngano, Shairi, zabibu, mchele, tende na zinginezo miongoni mwa nafaka zinazo pendwa zaidi, au ulipe thamani ya pesa inayo lingana na kiwango hicho, ni wazi kua thamani yake inatofautiana kutokana na kutofautiana kwa miji, kwa hiyo yampasa muumini aangalie thamani ya nafaka hizo katika mji wake kabla hajaamua kutoa pesa za thamani ya pishi.