Kikao cha Ramadhani (jioni) katika Atabatu Abbasiyya tukufu chahusisha jopo la wanahabari na wasimamizi wa msafara wa Alwafaa…

Maoni katika picha
Jioni ya Juma Nne (27 Ramadhani 1439h) sawa na (12 Juni 2018h) kimefanyika kikao katika Atabatu Abbasiyya tukufu kilicho husisha waandishi wa habari wa kiiraq na wasimamizi wa msafara wa Alwafaa unao toa misaada ya kibinadamu, ulio anzishwa na Atabatu Abbasiyya na kutekelezwa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji.

Kikao hicho kilitanguliwa na mambo mengine, kilitanguliwa na kutembelea makumbusho ya Alkafeel na kituo cha Alkafeel cha uzalishaji wa vipindi na matangazo ya moja kwa moja, kisha swala ya Maghribaini na kufturu pamoja na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ambaye alisisitiza umuhimu wa kutoa habari sahihi katika vyombo vya habari na kujiepusha na kutoa habari zisizo kua sahihi, akahimiza wajibu wa vyombo vya habari wa kutangaza matukio halisi, akasema kua nchi yetu inafursa nyingi ambazo zinatakiwa kutangazwa kwa walimwengu, inapasa kuonyesha utambulisho wetu wa kitaifa katika vyombo vyote vya habari, akaongeza kusema kua: “Hakika miongoni mwa mambo muhimu yanayo takiwa kuonyeshwa ni nafasi ya raia na uwezo mkubwa wa wananchi wa Iraq ambao tuna haki ya kujivunia, tunatakiwa kua watu wa kwanza katika kujenga taifa letu na kumaliza matatizo, kwa kua sisi ndio wenye nchi ni muhimu zaidi kufanya kazi hizo”.

Akasisitiza kuhusu: “Umuhimu wa kuwaenzi mashujaa wa fatwa tukufu ya kujilinda, na kuzijali familia za mashahidi na majeruhi, kwani mchango wao ni mkubwa sana katika kulinda amani na heshima ya Iraq, pia inawapasa watangazaji wa habari kutilia mkazo jambo la kuhimiza kuishi kwa amani baina ya watu mbalimbali katika jamii”.

Mwisho walifanya mazungumzo ya wazi pamoja na wasimamizi wa msafara wa Alwafaa yakiongozwa na Ustadh Maitham Zaidi yaliyo dumu saa moja na nusu, waliangazia mafanikio makubwa yaliyo patikana katika mfasara huo ulio anzia katika mji wa Basra hadi Mosul, pamoja na kuangalia malengo ya msafara huo.

Tunapenda kukumbusha kua lengo la kikao hiki, ni kutoa nafasi kwa vyombo vya habari kuangalia na kutambua mafanikio ya msafara wa Alwafaa unao toa huduma za kibinadamu, ulio anzishwa na Atabatu Abbasiyya na kutekelezwa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, sambamba ya mafanikio ya Ataba tukufu katika miradi ya ujenzi, utumishi, elimu na utamaduni.

Waandishi wa habari walionyesha kufurahishwa kwao na walicho kiona katika ziara hii, mwana habari bwana Alaa Khatwabu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Sisi tumefurahishwa sana na juhudi kubwa zinazo fanywa na Ataba tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, za kuendeleza ujenzi wa kisasa na kutoa huduma za kijamii hapa nchini, ni wazi kwetu kama wana habari maendeleo makubwa waliyo nayo Atabatu Abbasiyya tukufu katika kila sekta”.

Akaongeza kusema kua: “Jambo hili linaonyesha kuwepo kwa uongozi mzuri katika Atabatu Abbasiyya tukufu unao fanya kazi kwa bidii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: