Hivi punde.. Ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani yatoa wito kwa waumini kuwa makini katika kuangalia mwandamo wa mwezi mtukufu wa Shawwal…

Maoni katika picha
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema mwenye kurehemu.

Mtume (s.a.w.w) anasema: (Fungeni kwa kuonekana kwake na fungueni kwa kuonekana kwake).

Ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani katika mji wa Najafu inatowa wito kwa waumini wa Iraq na nchi za jirani kuwa makini katika kuangalia mwandamo wa mwezi wa Shawwal wa mwaka (1439h) baada ya kuzama jua siku ya Alkhamisi (29 Ramadhani tukufu).

Mtu yeyote atakaye uona mwezi mwandamo katika usiku huo, atowe ushahidi wa kuuona kwake moja kwa moja katika ofisi au kwa mawakili na Mu’tamadi (viongozi wa kidini) waliopo nchini.

Taarifa tulizo nazo kuhusu kuandama mwezi na uweko wake katika mbingu siku ya Alkhamisi, zinaonyesha kuna ugumu wa kuuona kwa macho moja kwa moja –bila kutumia telescop na vifaa mfano wa hicho- hapa Iraq na nhi jirani katika usiku huo, japo kua siku inayo fuata utaonekana ukiwa juu na mkubwa pia utakaa kwa muda mrefu.

Hivyo tunawahimiza waumini watukufu wajitahidi kuangalia mwezi jioni ya Alkhamisi hasa wale ambao anga litakua safi katika miji yao, Na Mwenyezi Mungu ni muwafikishaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: