Maqaamu Imamu Mahdi (a.f) ni moja ya vituo vya usomaji wa Qur’an vya Maahadi ya Qur’an ya Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba za usomaji wa Qur’an tukufu zilizo pangwa na Maahadi ya Qur’an chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, ni usomaji wa Qur’an katika maqaamu na mazaru tukufu za ndani na nje ya mkoa wa Karbala, miongoni mwa sehemu hizo ni maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f).

Usomaji huo wa Qur’an ni muendelezo wa usomaji ulio kua ukifanywa katika maqaamu hiyo toka zamani, na ni sehemu ya harakati za Maahadi ya Qur’an ya Ataba tukufu, zinazo lenga kueneza utamaduni wa Qur’an katika nyoyo za waumini na kuwafanya wafunganane na kitabu cha Mwenyezi Mungu wakati wote kwa kukihifadhi, kukisoma na kukitafsiri.

Usomaji huo unafanyika chini wa wasomi mahiri kwa kusoma juzuu moja kila siku na hushiriki kundi kubwa la watumishi pamoja na mazuwaru watukufu. Kumbuka kua Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba kamili ya usomaji wa Qur’an na mashindano ya Qur’an ndani ya Maahadi tukufu na katika matawi yake yaliyopo kwenye mikoa mbalimbali ya Iraq, kwa ajili ya kueneza utamaduni wa Qur’an tukufu na kuhakikisha Qur’an yote inasomwa katika mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: