Ofisi ya Marjaa dini mkuu: Juma Mosi ni mwezi mosi Shawwal siku ya kwanza ya Idil-Fitri tukufu…

Maoni katika picha
Ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani katika mji wa Najafu imewatangazia waumini watukufu kua, imekamilisha uchunguzi wa mwezi mtukufu wa Shawwal baada ya kuzama jua la leo Alkhamisi (29 Ramadhani), pamoja taarifa za kuandama mwezi kua nyingi lakini haijathibiti kisheria kuonekana mwezi kwa jicho hapa Iraq na miji ya jirani katika usiku huu, japo kua unatarajiwa unatarajiwa kesho utaonekana ukiwa juu tena kwa wazi zaidi, hilo haliufanyi kua wa siku mbili.

Fatwa ya Mheshimiwa Sayyid inasema kua mwanzo wa mwezi katika kila mji unategemea kuonekana mwezi kwa macho moja kwa moja, na wala haitoshi mwezi kuonekana katika nchi zingine, Ijumaa ya kesho tunakamilisha mwezi mtukufu wa Ramadhani na siku ya Juma Mosi ndio siku ya Idi-Fitri.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu apokee ibada za watu wote na awabariki katika sikukuu yao, aijaze heri na baraka hakika yeye ni mwenye kusikia mwenye kujibu.

Ofisi ya Sayyid Sistani / Najafu Ashrafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: