(Kwaheri kwaheri ewe mwezi wa Allah): Mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaaga mwezi wa Ramadhani katika usiku wa Ijumaa ya mwisho ndani ya mwezi huo…

Maoni katika picha
Katika uwanja mtakatifu wa kaburi la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika mazingira bora ya kiroho na kiimani, wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wanatumia usiku wa Ijumaa ya mwisho katika mwezi wa Ramadhani, usiku ambao utukufu wake na rehma zake hazielezeki, Mwenyezi Mungu mtukufu katika kila usiku wa mwezi wa Ramadhani huwaacha huru na moto watu laki moja, itakua vipi katika usiku huu mtukufu ambao waumini wanautumia kufanya ibada katika sehemu ambayo ni sehemu za udongo wa peponi, katika ardhi tukufu iliyo tukizwa na Mwenyezi Mungu, pembezoni mwa bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), wanajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu na kumuomba wakiwa katika ardhi hii takatifu, awakubalie funga zao na ibada zao, na awape thawabu kwa ibada hizi na zinginezo na wanafanya ibada za kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mazuwaru walianza kumiminika kwa wingi tangu baada ya Dhuhuraini (mchana) pamoja na kuongezeka kwa joto, wameendelea kufurika hadi karibia na wakati wa Maghribaini, chini ya ulinzi mkali na huduma bora kutoka kwa watumishi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) na kitengo cha uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, wamefanya kila wawezalo katika kutoa huduma nzuri zinazo endana na wingi wa mazuwaru watukufu, ili kuwawezesha kufanya ziara na ibada mbalimbali kwa amani na utulivu, ukizingatia kua usiku huu unaumuhimu maalumu, kwani ni usiku wa Ijumaa ya mwisho katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kupata fursa ya kufanya ibada na kuomba toba ni jambo kubwa sana, limepelekea watu kuja kwa wingi sana katika eneo hili tukufu na kutokea msongamano mkubwa wa mazuwari, hasa baada ya adhana ya Maghribi hadi karibia na katikati ya usiku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: