(Na katika riziki yako tumefuturu) mradi wa kufuturisha mazuwaru kila siku ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Harakati zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya mwezi wa Ramadhani ni nyingi sana, miongoni mwa harakati hizo ni kufuturisha, mradi unao itwa: (Na katika riziki yako tumefuturu), unao lenga kufuturisha mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambapo hugawa futari nyepesi kila siku karibia na mda wa swala ya Maghribaini kwa mazuwaru wote waliopo ndani ya ukumbi wa haram tukufu na wale waliopo katika sardabu, na katika baadhi za siku walikua wanapewa hadi waliopo nje ya haram tukufu.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa mradi huu, unao simamiwa na kitengo cha utumishi wakishirikiana na kitengo cha mgahawa (mudhifu), kazi hii ilianza mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, mradi huu umetokana na kufanyia kazi maneno ya Imamu Baaqir (a.s) yasemayo: (Muumini yeyote atakaye mfuturisha muumini siku moja ya mwezi wa Ramadhani, Mwenyezi Mungu atamuandikia thawabu sawa na mtu aliye muacha huru muumini), na akasema tena: (Na atakaye mfuturisha mwezi wote wa Ramadhani, Mwenyezi Mungu atamuandikia thawabu za kuacha huru waumini thelathini, na atakua anakubaliwa maombi yake).

Mazuwaru wanashauku ya kutabaruku kwa chakula hiki kidogo katika muonekano wake kikubwa kwa madhumuni yake, pia watumishi wanashindana katika kutoa huduma hii, ambayo huanza mapema kila siku, na katika usiku wa Ijumaa huwanza mapema sana ili waweze kugawa kwa urahisi.

Kwa hakika huduma hii ni sawa na huduma mbili kwa wakati mmoja, huduma ya kwanza ni kupata utukufu wa kumhudumia zaairu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na huduma ya kumfuturisha aliye funga, yenye malipo na thawabu zisizo elezeka, idadi ya wanufaika wa huduma hii ni kati ya watu (3000) elfu tatu katika siku za kawaida, hadi watu (10,000) elfu kumi katika usiku wa Ijumaa, na siku za minasabaati na za Lailatul Qadri.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba maalumu ya ulinzi na utoaji wa huduma katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, yenye vipengele vingi, na wanaifanyia kazi ratiba hiyo kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru na kuwarahisishia utekelezaji wa ziara na ibada zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: