Kuwazawadia washiriki wake: Maahadi ya Qur’an tukufu yahitimisha ratiba ya usomaji wa Qur’an tartiil katika mwezi wa Ramadhani…

Maoni katika picha
Jirani na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika mazingira bora ya kiroho na kiimani, jioni tukufu ya siku ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani, Maahadi ya Qur’an tukufu imekamilisha moja ya ratiba zake muhimu ndani ya mwezi wa Ramadhani ambayo ni usomaji wa Qur’an tartiil, iliyo dumu mwezi mzima chini ya wasomi mahiri wa kimataifa.

Hafla ya ufungaji ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na Mustwafa Ghalibi, ukafuata usomaji wa kikundi cha wasomi walio shiriki katika ratiba ya usomaji ndani ya mwezi wa Ramadhani, ambao walisoma nusu ya mwisho ya juzuu la thelathini, halafu ukafuata ujumbe wa wasomaji washiriki ulio wasilishwa na Shekh Maitham Tammaar, alitoa shukrani kwa Atabatu Abbasiyya kupitia Maahadi ya Qur'an tu’ufu, kwa kuwaita katika meza ya usomaji wa Qur’an ndani ya ukumbi wa bwana wa maji, ili washindane katika usomaji wa Qur’an mbele ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s).

Misho kabisa wakapewa zawadi wale walio shiriki katika ratiba ya usomaji wa Qur’an ndani ya mwezi wa Ramadhani, ambayo ni sehemu muhimu katika ratiba ya Atabatu Abbasiyya ya mwezi wa Ramadhani.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya iliandaa ratiba maalumu ya usomaji wa Qur’an katika mwezi wa Ramadhani, ndani ya Maahadi na katika matawi yake yaliyo enea katika mikoa mingi ya Iraq, kwa ajili ya kusambaza utamaduni wa usomaji wa Qur’an na kuwezesha kusomwa Qur’an yote ndani ya mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: